Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, October 2, 2015

NEC yatoa uhuru kwa waandishi siku ya uchaguzi!

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, Ramadhani Kailima
By Hamida Shariff, Mwananchi
Morogoro. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) itaruhusu waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kufika kwenye vituo vya kupigia kura na kufanya mahojiano na wapiga kura pamoja na wasimamizi wa uchaguzi kuhusu zoezi la kupiga kura litakavyokuwa likiendelea.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa NEC, Ramadhani Kailima wakati wa mafunzo ya siku mbili ya waratibu wa uchaguzi, wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya majimbo na wilaya na maafisa wa uchaguzi yaliyofanyika mjini hapa.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni wa kihistoria kwani kwa mara ya kwanza waandishi wa habari wataruhusiwa kufika katika vituo vya uchaguzi kwa lengo la kupata habari kutoka kwa wasimamizi wa uchuguzi na hata wapiga kura kuhusu namna uchaguzi huo unatotarajiwa kufanyika Oktoba 25 utakavyokuwa ukiendelea.
Hata hivyo Kailima amesema kuwa kwa sasa tume inaandaa mwongozo utakaoeleza taratibu na mipaka ya waandishi wa habari pamoja na watakaohusika kutoa habari katika vituo hivyo vya kupigia kura.
Katika hatua nyingine Kailima amesema kuwa NEC imepata taarifa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa  (TMA) iliyotabiri kuwa mwezi Oktoba kutakuwa na mvua hivyo NEC imejiandaa kukabiliana na changamoto hiyo.
Hivyo amewataka wasimamizi wa uchaguzi kubaini mapema maeneo ambayo yanaweza kuingia maji na kuweka tahadhari ili kuepuka usumbufu kwa wapigakura ama uharibifu wa vifaa vya kupigia kura zikiwemo karatasi.

No comments :

Post a Comment