Jeshi la Polisi
Jeshi la polisi nchini, limesema limenunua mitambo mingi ya kukabiliana na watu wanaokiuka sheria za uhalifu katika mitandao na miamala ya kielektroniki.
Akizungumza katika kikao cha watekelezaji wa sheria za makosa ya mtandao na miamala ya kielektroniki za mwaka 2015 jijini Mwanza jana, Mwanasheria wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, Alfred Honga, alisema baada ya sheria hiyo kupitishwa Aprili mosi, mwaka huu, jeshi lilijenga uwezo kwa polisi wake ili kukabiliana na uhalifu huo.
Jeshi lilifanikiwa kununua mitambo ya kutosha baada ya baada ya sheria hiyo kupitishwa ili kuweza kukabiliana na wahalifu na kupunguza matukio mitandaoni, alisema Haonga.
Alisema mitambo hiyo ni pamoja namtu aliyejirekodi kwa sauti tofauti, kutambuliwa.
Haonga alisema mafanikio ambayo yamepatikana baada ya sheria hiyo kuanza kufanya kazi ni kupungua kwa matumizi ya lugha za hovyo mitandaoni pamoja na picha zisizofaa katika jamii kuwekwa hadharani.
Awali hakimu mkazi wa wilaya ya Meatu, Pius Mabula, alisema kabla ya sheria hiyo kupitishwa walikuwa wakipata shida ya kutoa maamuzi kwa watu waliopatikana na hatia ya makosa ya mtandaoni.Naye mwanasheria wa wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Eunice Masigati, alisema wizara imejipanga kupitia mawasiliano ili kuweza kukabiliana na wanaokiuka sheria za mitandao.
Alisema kabla ya sheria hiyo kupitishwa na Bunge Aprili mwaka huu, ilikuwa vigumu kuwatia hatiani watu waliokuwa wakitumia vibaya mitandao ya kijamii kwa kuweka picha za ngono za watoto, kutukana na meseji za uongo.
Akifungua mkutano huo, Prisca Ulomi kwa niaba ya Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, John Mngodo, alisema lengo la kukabiliana na changamoto za makosa ya kimtandao.
Alisema makosa hayo ni kama wizi, uchochezi, udhalilishaji, usambazaji wa picha za utupu ama matusi ambayo awali serikali ilikuwa haina sheria ya kusimamia makosa hayo.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment