dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, October 14, 2015

Tuutumie Uchaguzi Mkuu kumuenzi Mwalimu Nyerere

NA EDITOR

14th October 2015.
Katuni.
Watanzania leo wanaadhimisha miaka 16 ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere. Mwalimu Nyerere alifariki dunia jijini London, Uingereza Oktoba 14, 1999.
 
Katika kumbukumbuka siku hiyo ya majonzi kwa taifa, shughuli mbalimbali zimekuwa zikifanyika zikiwamo maombi, mikutano, makongamano, midahalo kwa kutaja baaadhi.
 
Katika shughuli hizo, miongoni mwa mambo ambayo yamekuwa yakizungumzwa ni aliyofafanya na kuyasimamia Mwalimu Nyerere wakati wa uhai wake kwa taifa letu.
 
Mwalimu Nyerere alifanya mambo mengi mazuri ambayo yanakumbukwa na Watanzania, Afrika na duniani kote. Ni mambo hayo ambayo kila inapofika kumbukumbu ya kifo chake yamekuwa yakijadiliwa kwa mapana, huku msisitizo ukiwa ni kutaka mambo hayo yaenziwe. Katika mijumuiko hiyo, makundi kadhaa katika jamii yamekuwa yakiwalaumu viongozi wa serikali na wa kisiasa kwa kushindwa kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kufuata misingi yake ya uongozi.
 
Kwa ujumla, Mwalimu Nyerere alilifanyia taifa hili mambo mengi mazuri na kukumbukwa, kuanzia kusaka uhuru wa Tanganyika uliopatikana mwaka 1961 na kufuatiwa na kuweka misingi ya kuifanya nchi ijitegemee, yenye umoja, mshikamano na amani.
 
Mwalimu aliainisha maadui watatu wa Taifa baada ya uhuru kuwa ni ujinga, maradhi na umaskini na kuiona njia ya kufikia mafanikio kuwa ni itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea ambayo ilianza kutekelezwa kwa vitendo kupitia Azimio la Arusha mwaka 1967.
 
Mambo aliyoyapa kiupambele ni elimu ambayo ilitolewa bure kuanzia shule za msingi hadi chuo kikuu pamoja na huduma za afya.
 
Kilimo pia kilipewa msukumo mkubwa kwa kuamini kuwa kilikuwa kimeajiri asilimia kubwa ya wananchi na kuwa sekta iliyoongoza kwa kuingiza pato kubwa kwa taifa.
 
Mwalimu alinzisha viwanda vingi sambamba na mashirika ya umma takribani 400, lengo likiwa kutoa ajira kwa wananchi pamoja na kuingiza fedha za kigeni. Kwa ujumla wananchi wengi walinufaika.
 
Mwalimu pia atakumbukwa kwa mchango wake wa kuweka msingi imara wa ujenzi wa umoja wa taifa kwa kupiga vita ukabila, udini, ukanda, rangi na jinsia. Ndiyo maana tunaitana Watanzania.
 
Kwa kuweka misingi hiyo nchi yetu ilidumu katika amani na pale vilipoonekana viashiria vya kuharibu amani, hakusita kujitokeza hadharani na kuvikemea kwa nguvu zote bila kujali nani walihusika.
 
Tunapoadhimisha kumbukumbu ya  miaka 16 ya kifo cha Mwalimu Nyerere mwaka huu, Watanzania  hatunabudi kuenzi amani na umoja wa taifa letu kwa kuzingatia kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu.
 
Kwa kutambua kuwa machafuko vurugu katika nchi nyingi chanzo chake ni uchaguzi, tunamshauri kila mmoja wetu atimize wajibu wake kwa lengo la kuhakikisha kwamba uchaguzi huo unafanyika katika mazingira ya amani na utulivu.
 
Aidha, tunawakumbusha wadau muhimu wa uchaguzi wakiwamo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), vyama vya siasa, vyombo vya dola na wagombea wenyewe waheshimu na kufuata sheria za nchi ili uchaguzi huo uwe huru na wa haki.
 
Kwa kuwa kampeni zinazoendelea zimeonyesha dalili za wakati mwingine kukosekana kwa ustaarabu na busara kutokana na baadhi ya wapambe kutumia kauli za matusi, kashfa na uzushi, tunaamini kuwa kama kweli wanamuenzi Mwalimu Nyerere, watabadilisha mikakati yao ya kuwaomba kura kwa kujenga hoja za ushawishi.
 
Tunawashauri wagombea watoe ahadi zinazoweza kutekelezeka zikiwamo za kuboresha maisha ya wananchi. Ahadi hizo zilenge maeneo ambayo yanaweza kuwapunguzia kama siyo kuwaondolea wananchi umaskini.
 
Tunasema hivyo, kwa kuwa licha ya Mwalimu Nyerere kuanzisha mikakati ya kuondoa umaskini tangu baada ya uhuru, mipango yake mingi haikutekelezwa na kusababisha kuongezeka kwa umaskini kwa kasi kubwa kwa wananchi walio wengi.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment