Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, October 3, 2015

Mkutano wa wauguzi wasitishwa ghafla!

http://www.zanzibarnikwetu.blogspot.ca/2015/10/madaktari-wauguzi-wafamasia-pamoja-na.html


  •  Mkutano huo uliokuwa umalizike jana kwa kufanya uchaguzi, ulianza kuingia dosari asubuhi baada ya viongozi kuchukuliwa na maofisa usalama na kurejeshwa baada ya saa kadhaa huku wakisindikizwa na gari la Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera.
By Phinias Bashaya, Mwananchi
Bukoba. Mkutano mkuu wa Chama cha Wauguzi Tanzania (Tana), uliokuwa unaendelea mjini Bukoba umesitishwa chini ya ulinzi wa polisi, ikiwa ni siku moja baada ya viongozi wao kutoa tamko linalotaka kuwapo kwa mabadiliko katika sekta ya afya.
Mkutano huo uliokuwa umalizike jana kwa kufanya uchaguzi, ulianza kuingia dosari asubuhi baada ya viongozi kuchukuliwa na maofisa usalama na kurejeshwa baada ya saa kadhaa huku wakisindikizwa na gari la Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera.
Baada ya vingozi hao kurejeshwa wauguzi walikusanyika katika viwanja vya mkutano St. Theresa huku Rais wa Tana, Paul Magesa akisema baada ya kushauriwa wamelazika kuahirisha mkutano huo kwa sababu za kiusalama.
Alisema mkutano huo unaahirishwa hadi watakapotangaziwa tena na kuwa hata sherehe iliyokuwa imeandaliwa haitafanyika.
Baada ya maelezo ya Magesa, alifuata Kaimu mkurugenzi wa Ukunga na Uuguzi nchini, Ama Kasangara ambaye alisisitiza suala la kuahirishwa kwa mkutano huo na wauguzi kuondoka.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongela alisema jana kuwa taarifa za kusitishwa mkutano huo anazo ila hakuzifanyia kazi.
Mongela aliyekuwa mgeni rasmi wakati tamko la mabadiliko linatolewa, alisema ni kweli walizungumzia suala hilo wakilenga kero zinazowakabili wauguzi katika sekta ya afya, lakini siyo kwa maana ya kisiasa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi alisema tukio la polisi kuwapo eneo hilo ni jambo la kawaida kama wanavyofanya katika mikutano mingine huku akisisitiza kuwa hawajafunga mkutano na kwamba ajenda iliyofanya kuahirishwa ni kuhusu uchaguzi.
Ollomi alikataa kuzungumzia kuharishwa kwa mkutano huo kama kuna uhusiano na kauli ya mabadiliko katika sekta ya afya.
Mkutano huo wa siku tatu uliokuwa na lengo la kuwachagua viongozi wa chama hicho na kubeba kaulimbiu iliyosema: “Wauguzi ni nguzo ya mabadiliko katika kuleta huduma bora kwa gharama nafuu,” ulitakiwa kumalizika jana jioni.
Baadhi ya wauguzi nchini waliokuwa wamehudhuria mkutano huo walisema wameshtushwa na hatua ya kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu baada ya viongozi wao kupotea kwa muda.

No comments :

Post a Comment