Tarehe 22 Oktoba, 2015, baada ya Mhe. Balozi Jack Mugendi Zoka kuwasilisha Hati za Uwakilishi kwa Mhe. Salvador Mesa, Makamu wa Rais wa Cuba, aliandaa hafla fupi aliyowaalika Mabalozi wanaoziwakilisha nchi za Africa nchini Cuba, mabalozi viongozi wa Kanda mbalimbali na baadhi ya viongozi wa serikali ya Cuba.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na wanafunzi wa Kitanzania wanosomea Udaktari kwenye Chuo Kikuu cha Latin American School of Medicine kilichopo Havana.
Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka akitoa hotuba fupi kwa waalikwa (hawapo pichani)wakati wa hafla aliyoiandaa katika sherehe za kuwasilisha hati za Utambulisho nchini Cuba. Katikati ni Mama Baloz, Esther Nyanzila Zoka na kulia ni mkalimani.
Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka (katikati) akiwa pamoja na mabalozi wenzake wakati wa hafla aliyoiandaa katika sherehe za kuwasilisha hati za Utambulisho nchini Cuba.
Wageni waalikwa, mabalozi wanaowakilisha nchi zao Cuba na viongozi mbalimbali wa serikali ya Cuba wakiwa katika hafla iliyoandaliwa na Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka.
Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka (wa pili kutoka kushoto) akibadilishana mawili-matatu na mabalozi wenzake wakati wa hafla aliyoiandaa katika sherehe za kuwasilisha hati za Utambulisho nchini Cuba.
Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka (wa pili kutoka kushoto) akiwasikilza mabalozi wenzake wakati wa hafla aliyoiandaa katika sherehe za kuwasilisha hati za Utambulisho nchini Cuba.
Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka (wa kwanza kutoka kulia) akiwa pamoja na wanafunzi wa Kitanzania wanaosomea udaktari katika Chuo Kikuu cha Latin American School of Medicine, Havana, wakati wa hafla aliyoiandaa katika sherehe za kuwasilisha hati za Utambulisho nchini Cuba.
Baadhi ya wanafunzi wa Kitanzania wanaosomea udaktari katika Chuo Kikuu cha Latin American School of Medicine, Havana, wakati wa hafla aliyoiandaa katika sherehe za kuwasilisha hati za Utambulisho nchini Cuba.
Picha ya pamoja. Kutoka kulia ni Mama Balozi, Esther Nyanzila Zoka, Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka, Afisa wa Mambo ya Nje wa Cuba anayeshughulikia masuala ya Afrika, Afisa wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bw. Paul James Makelele, mwanafunzi wa Kitanzania anayesomea Udaktari, Cuba, Mangaro Mabusi na mkalimani.
Picha ya pamoja. Ujumbe wa Mhe. Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka na wanafunzi wa Kitanzania wanaosomea udaktari katika Chuo Kikuu cha Latin American School of Medicine, Havana
No comments :
Post a Comment