Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, November 1, 2015

Bei ya bidhaa yapanda Zanzibar!


By Salma Said, Mwananchi.
Zanzibar. Hali ya uchumi Zanzibar inazidi kudorora huku bei za bidhaa zikizidi kupanda kutokana na meli zinazosafirisha bidhaa hizo kutoka Tanzania Bara kupunguza safari zake kutokana na hali ya kisiasa iliyopo hapa Zanzibar.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wafanyabiashara katika masoko ya Darajani na Mwanakwerekwe Mkoa wa Mjini Magharibi wamesema wanalazimika kupandisha bei kutokana na bidhaa zinazoingia kupanda bei.
“Gunia la viazi mbatata tulikuwa tukilinunua Sh100,000 lakini sasa tunanunua kwa Sh250,000 unategemea tutauza kiasi gani, lazima tuuze kilo moja Sh1,500 hadi 2,000 badala ya Dh800,” alisema Abdi Sulaiman.
Nasoor Khalid alisema bidhaa kama maharage, kunde, mbaazi ambazo husafirishwa kutoka Tanzania Bara hazipatikani kutokana na safari za meli kupungua, jambo ambalo alisema linawasumbua wanaozihitaji.
“Bidhaa zangu zinatoka Mbeya, Arusha na Ifakara na hadi zifike Zanzibar, inachukua siku mbili au tatu lakini tokea kumalizika uchaguzi imekuwa ngumu kupata bidhaa hizo afadhali bidhaa za nafaka hununuliwa sana Mwezi wa Ramadhani kwa hivyo afadhali kidogo wanaohitaji sio wengi kwa sasa” aliongea Khalid.
Kwa upande wa wauzaji wa vitoweo kama nyama, samaki, dagaa na mboga za majani nazo hazijasalimika kutokana na upatikanaji wake kuwa mgumu, hasa zile zinazotoka Tanzania Bara.
Mbogamboga za majani kama bamia, chicha, kabichi, nyanya (tungule), vitunguu saumu na vitunguu maji nazo zimeadimika na kupanda bei katika masoko ya Zanzibar.
“Tungule (nyana) kilo moja  ilikuwa inauzwa Sh1,500 lakini sasa kilo moja Sh3,000, nyama kilo moja Sh12,000 badala ya bei yake ya kawaida Sh8,000 kwa kweli bidhaa zimepanda bei sana na wananchi hawawezi kununua hizo bidhaa,” alisema Mohammed Suleiman ambaye ni muuza Nyama katika Soko Kuu la Darajani.
Kwa upande wa wauzaji wa Soko la Mwanakwerekwe ambao baadhi ya bidhaa huchukua mashamba wanasema wanalazimika kupandisha bei kutokana na hali ya usalama kuwa tete kila mtu anaogopa kuleta bidhaa zake Mjini ingawa wanajua zinaweza kununuliwa na kumalizika lakini khofu ya usalama ianwatia wasiwasi.
“Sio kwamba hatutaki kuleta viti kuuza Mjini lakini hali haijatengemaa njia kila wakati zinafungwa majiani lakini pia hizo gari zinazozunguka za vikosi na kupiga mabomu ya machozi kila pahala nayo ni mambo yenye kuturejesha nyuma” alisema Nyange Makame mletaji bidhaa kutoka Kaskazini Unguja.
Bidhaa kama Ndizi, Mihogo na Mabungo ambayo huletwa kutoka Kisiwani Pemba  nazo zimeadimika kutokana na waletaji wa bidhaa wamepunguza kuleta bidhaa zao Kisiwani Unguja kutokana na hali tete.
“Ndizi moja shilingi 1.000 hadi 1.500 na wakati mwengine unapata 5 unaweza kupata kwa shilingi 15 na ndizi zenyewe ndogo kabisa” alisema mnunuzi Asha Abdulrahman.
Fatma Said Mohammed anasema wanaogopa kwenda kununua bidhaa kutokana na hali ilivyo kwani wanahitaji bidhaa lakini kutokana na hali ya wahka wanaogopa kwenda madukani na kununua vitu.
“Bidhaa zimepanda bei sana lakini pia kuna tatizo hili la kiusalama kuna hali ya khofu kila mmoja amepatwa na khofu anaogopa kutoka vyakula vyetu vishamaliza majumbani lakini mtu anaogopa kutoka nje na wakenda wananunua na kukimbia haraka kurudi nyumbani huko kila wakati Darajani mara magari ya jeshi mara mapolisi khofu tupu” amesema Fatma.
Wananchi mbali mbali waliozungumza na Gazeti hili wanaiomba serikali kumaliza suala la uchaguzi na kurejesha hali ya usalama Zanzibar ili wananchi wapate kurudi katika hali zao za kawaida kwani kutokana na maisha yalivyopanda hawawezi kuhimili hali hii ya uchumi.

No comments :

Post a Comment