“Nachukua uongozi wa taifa nikiwa nasononeshwa na mpasuko wa kisiasa kati ya Unguja na Pemba na pengine kati ya Pemba na sehemu nyingine za Jamhuri yetu,” alisema na kuongeza;
“Wakati umefika wa kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa mpasuko huo. Nategemea kupata ushirikiano mzuri kutoka kwa wanasiasa wa pande zote wa Zanzibar. Naomba mnielewe dhamira yangu.”
“Nakusudia kufanya kila lililo ndani ya uwezo wangu ili siku awamu yangu ya uongozi wa Jamhuri yetu ikifika ukingoni nisiiache hali hii ya mpasuko wa kisiasa kama nilivyoikuta.”
Ni kutokana na dhamira hiyo njema ya Rais Kikwete, tulishuhudia vyama vya CUF na CCM vikiunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).
Katika hotuba yake ya kulivunja Bunge aliyoitoa Julai 9, 2015, Rais Kikwete alisema kuundwa kwa SUK kulifanya mpasuko wa kisiasa uliodumu tangu uchaguzi wa mwaka 1995 kupatiwa tiba.
Leo Rais Kikwete akiwa katika siku za mwisho za utawala wake, anataka kuondoka akiiacha Zanzibar katika mtafaruku mkubwa wa kisiasa baada ya watawala kugoma kumtangaza mshindi!
Bahati mbaya, watawala wetu wameweka sheria mbaya ambazo haziruhusu mtu yeyote kuhoji ushindi wa mgombea urais kama ametangazwa na Tume ya Uchaguzi.
Ibara ya 41(7) ya Katiba ya 1977 inasema” Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kuwa Rais, hakuna mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake”.
Kifungu cha 34 (7) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, nacho kimeweka kifungu kama hicho cha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinachozuia kuchunguza kuchaguliwa kwa Rais.
Sheria hizi ni mbaya kwa kuwa kama kutatokea mgogoro wa kisiasa, hakuna njia ya kuweza kutokea. Tumejenga nyumba tukaweka mageti na kuziba kila mahali.
No comments :
Post a Comment