Katika Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na viongozi wa Wilaya na Majimbo wa Chama hicho katika Ukumbi wa Majid, Kiembesamaki Zanzibar.
Viongozi wa Wilaya na Majimbo wa CUF, wakimsikiliza katiba mkuu wa Chama hicho Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad katika Ukumbi wa Majid, Kiembesamaki Zanzibar.
Mwenyekiti wa kamati ya Uongozi CUF Taifa Bw. Twaha Taslima, akisoma maazimio ya baraza kuu kwa waandishi wa habari katika ofisi za Chama hicho Vuga mjini Zanzibar. (Picha na Salmin Said, OMKR).
Na: Hassan Hamad, OMKR
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amewataka wafuasi na wapenzi wa Chama hicho kutembea kifua mbele kutokana na ushindi mkubwa walioupata katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 25 mwezi uliopita.
Amesema ushindi huo umeleta matumaini mapya kwa wazanzibari ambao wameitumia vyema haki yao ya kupiga kura na kuwachagua viongozi wanaoataka.
Akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu ngazi za Wilaya na Majimbo katika ukumbi wa Majid Kiembesamaki Zanzibar, Maalim Seif amesema hakuna namna yoyote ya kupindua maamuzi ya wananchi waliyoyafanya kupitia masanduku ya kura.
Amesema wanachokifanya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar hivi sasa ni kuchelewesha kukamilisha uhakiki wa kura kwa majimbo 14 yaliyobakia na kumtangaza mshindi wa Urais, na hivyo kuishauri tume hiyo kukamilisha zoezi hilo ili serikali mpya ianze kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi.
“Mimi sina wasi wasi, ninajihesabu kama Rais ninayesubiri kuitwa na kuapishwa, na sasa nimo katika matayarisho ya kuunda serikali ili nikiapishwa tu nisipoteze tena muda wa kufikiria kuunda serikali”, alisema Maalim Seif katika kikao hicho cha kwanza cha kuzungumza na wajumbe hao tangu uchaguzi mkuu wa Zanzibar ulipomalizika.
“Mimi sina wasi wasi, ninajihesabu kama Rais ninayesubiri kuitwa na kuapishwa, na sasa nimo katika matayarisho ya kuunda serikali ili nikiapishwa tu nisipoteze tena muda wa kufikiria kuunda serikali”, alisema Maalim Seif katika kikao hicho cha kwanza cha kuzungumza na wajumbe hao tangu uchaguzi mkuu wa Zanzibar ulipomalizika.
Amesema tayari dunia nzima wanamfahamu Rais aliyechaguliwa na wananchi wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu uliopita, na kuwataka wanachama wa Chama hicho kuacha kusikiliza kile alichokiita proganda za Chama Cha Mapinduzi zinazoeleza kurejewa kwa uchaguzi.
Amefahamisha kuwa hakuna sababu za kurejewa kwa uchaguzi huo kwani uchaguzi ulishakamilika katika ngazi zote na washindi wa uwakilishi na udiwani kutangazwa bila ya kuwepo malalamiko yoyote, na kwamba kinachosubiriwa hivi sasa ni kukamilika kwa zoezi la uhakiki wa kura za Urais kwa majimbo yaliyobakia na hatimaye mshindi wa uchaguzi huo aweze kutangazwa.
Akizungumzia madai ya ongezeko la kura katika kisiwa cha Pemba, Maalim Seif amesema madai hayo hayana ukweli kwani hakuna hata kituturi kimoja kilichozidishwa wapiga kura 350 kiliwopangiwa na kwamba vituturi vingi vilikuwa na wapikura chini ya idadi hiyo.
Mapema akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mipango na Chaguzi wa CUF Omar Ali Shehe, amesema licha ya ushindi wa Urais, Chama hicho pia kimepata ushindi mkubwa kwa nafasi za Uwakilishi na Udiwani.
Amesema katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 Chama hicho kilipata Wawakilishi wanne (4) na madiwani saba (7) kwa upande wa Unguja ambapo uchaguzi wa 2015 kimefanikiwa kupata Wawakilishi tisa(9) na madiwani kumi na tano (15).
Aidha amesema Chama Cha Mapinduzi kimepoteza wodi zote tatu (3) za udiwani katika kisiwa cha Pemba na kukifanya Chama hicho kushindwa kupata mjumbe yeyote wa Baraza la Wawakilishi, Ubunge na Udiwani.
Kabla ya mkutano huo, Baraza Kuu la Uongozi CUF chini ya Mwenyekiti wake ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama hicho Taifa Bw. Twaha Taslima, liliitisha mkutano wa waandishi wa habari kueleza maazimio ya baraza hilo kufuatia kikao chake cha dharura kilichokutana jana 07/11/2015 katika hoteli ya Mazsons Mjini Zanzibar.
Katika maazimio yake Chama hicho kimeishauri Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutengua uamuzi wa mwenyekiti wake Bw. Jecha Salim Jecha wa kufuta uchaguzi mkuu wa Zanzibar, kwa vile hana mamlaka ya kikatiba na sheria ya uchaguzi kuweza kufuta uchaguzi huo.
/ZanziNews.
No comments :
Post a Comment