Mimi namuomba, Mheshimiwa Rais mteuliwa, kwa heshima na taadhima hili ni ombi binafsi kwako.
Nnaomba uhakikishe huyu mrembo wa ACT Bi Anna Mughwira unamuingiza bungeni na unampa wadhifa anaostahiki, huyu mama ni kichwa adhyim na adim kabisa.
Nimemfatilia mikutano yake mingi sana ya kampeni, anatoa vitu kichwani utafikiri ana word processor inayopanga na kuchuja anachokizungumza kutoka kichwani bila kusoma.
Halikadhalika leo kanifurahisha sana alipostukizwa na kutoa hotuba pale Diamond, ilikuwa fupi na imelenga points zote nzuri na ameeleweka vyema kabisa.
Anna heko sana na nitakuunga mkono katika siasa zako.
\
Ili kuipa hadhi na kuitangaza lugha yetu ya taifa, nashauri rais wetu mpya atumie Kiswahili katika shughuli zote rasmi za kitaifa na kimataifa. Cha msingi ni kuwa na wakalimani mahiri katika shughuli za kimataifa. Hii itainua hadhi na heshima ya nchi yetu badala ya kuendelea kuthamini lugha za kigeni. Tumekuwa watumwa mno wa lugha ya kiingereza mpaka kufikia hatua kudhani kuwa mtu anayeongea kiingereza vizuri ndiye aliye elimika wakati si kweli. Elimu ni uwezo siyo kuongea kiingereza. Hiki kiingereza cha "izi, wozi, wea, kongrugesheni, ameizingi, wati?, yu no, no problemu hakitusaidii kitu. Na kwa ujinga wetu tunafundishana kwa lugha tusiyoijua vizuri matokeo yake watoto wanafeli halafu tunawaona wajinga kumbe sera zetu ndio mbovu. Wachina, wakorea, wajerumani, wareno, wafaransa mbona wanatumia lugha zao na wanapiga hatua kubwa sana katika uchumi na sayansi. Sisi na kiingereza chetu cha kuombea maji tumefika wapi zaidi ya kutudhalilisha?
Maoni yangu haya hayana maana kuwa sitambui uwezo mkubwa wa kiingereza alio nao dr. Nataka aendeleze pale mwenzake alipoachia mwenzake, kwani alianza kwa kuhutubia kwa kiswahili kwenye mkutano wa AU lakini baadaye akaacha. Mimi nashauri Dr. sasa ajikite pamoja na mambo mengi kuitangaza lugha ya kiswahili kimataifa kwa yeye mwenyewe kuitumia badala ya kiingereza. Huwa naona viongozi wa nchi nyingine kama za kiarabu pamoja na kuwa wanajua kiingereza lakini utakuta wanazaunguza kiarabu na kisha wasiojua kutafsiriwa. Wakalimani sasa hivi tunao wengi, ni vizuri wakatumika vizuri kuikuza lugha yetu ya taifa. Ukweli ni kuwa unapotumia lugha mama au lugha ya taifa una kuwa na uhuru na uwezo mkubwa sana wa kujieleza na kuelezea kuliko unapotumia lugha za kigeni. Kwa watanzania wengi lugha yetu ya mama ni kiswahili.Jambo moja ambalo Magufuli aliliona wazi katika kampeni zake ni kwamba Watanzania wanataka mabadiliko, na kwamba wengi walihisi mabadiliko haya yangeletwa na UKAWA. Magufuli akaahidi kwamba yeye ataleta madadiliko Watanzania wanayotaka.
Ushauri wangu kwa Magufuli ni kwamba kama kweli kweli anataka kuwaletea Watanzania mabadiliko - basi asiwe mtu wa kutafuta ushari kwa Kikwete na Mkapa. Wao walikuwa na nafasi ya kuletea Watanzania mabadiliko, na wengi waliona kuwa kwa sehemu kubwa walishindwa kuleta mabadiliko yaliyotakiwa, japo kulikuwa a mafanikio kataka sehemu chache.
Magufuli be your own man and master - Personality yako, kufikiri kwako na kule kwa kwa Kikwete na Mkapa ni tofauti kabisa na Watanzania wanategemea hilo litaleta mabadiliko wanayotarajia. Kuendelea kupokea ushauri toka kwa Kikwete na Mkapa ni kuwapa Watanzania mvinyo ule ule wa zamani katika glasi mpya; hilo ni hatari sana, na linaweza kukufanya uongoze kwa miaka mitano tu na kushindwa uchaguzi ujao.
Tunajua Kikwete a Mkapa walikuwa na mchango kukufanya uwe Raisi wa Tanzania - washukuru yaishie hapo. Waambie wakapumzike sasa, kazi yao imekwisha. Kuendelea kupokea ushauri wao kila wakati utajikuta unafanya kazi ili kuwaridhisha wao na sio Watanzania waliokuchagua. Pia epuka sana kupokea ushauri wao kwa mambo ambayo hujawaomba ushauri.
Lakini kuwa na washauri ni jambo nzuri tu - ila sasa tafuta washauri wako mwenyewe, watu wasio rafiki zako ambao wanaeleweka kuwa na busara na uzoefu katika uongozi, bila kuwa na haja ya kukufurahisha wewe kibinafsi, kutafuta urafiki na wewe au kujipendekeza kwakoUchaguzi ulisha kwisha good enough tuna katiba ambayo inasema mtu akishwa tangazwa basi ndiyo raisi na huna uwezo wa kupinga matokeo hayo popote its good when it is your turn but mind you atakuja tokea chizi mmoja me or ke ambaye ataamua kumuingiza mkewe au mmewe kwa kujua siku ya siku yeye ndiye mwenye mamlaka ya kutangaza matokeo ya urais atamtangaza spouse wake kutakucha, tuyaache hayo.
Binafsi kama ningepata wasaa wa kuongea na magufuli ningemshauri haya yafuatayo
1. Hali ya hudumu ya afya ya Tanzania ni mbaya mbaya mbaya hakuna daktari aliye na moyo wa kufanya kazi kwa moyo ule uliokuwapo mwanzo. Mfano, hospitali yetu ya taifa ambayo ni tegemeo ya maskini wote wa Tanzania na daraja la viongozi kupita kwenda India huduma ni hovyo hovyo.
Hivi unajua kuwa huduma za CT Scan na MRI Muhimbili zimesimama Zaidi ya miezi minne na hakuna anayejali. Watu wa wizara ya afya naona hawajali kabisa.
Mimi nashauri wizara ya afya isihusike moja kwa moja na Muhimbili kama mtafuta habari nilienda pale, hakuna mwenye nia za dhati wa kuikomboa sekta ya afya.Wao wanachotaka serikali iendelee kupeleka watu India ili waendelee kupata pesa wanazopata wanajua namna wanavyopata, si watu hawa tunakufaa maskini.
2.Taasisi ya mifupa MOI tunaomba ijipambanue kama ni taasisi ya umma au ni kama Agha Khan kwani huduma zinazotolewa hapa afadhali malipo yake yangekuwa na risiti basi ni ujanja ujanja tu.
Heri na feri kwenye soko la samaki kuliko hapo, elimu yao haifanani na huduma wanazotoa.
Mimi naomba kama kama una power hiyo hizi taasisi ziwe chini yako kwani afya ya watu unaowaongoza ni muhimu saaana tena sana elimu ifuate.Tanzania sasa tumempata Rais mpya wa awamu ya 5, ambaye watanzania wengi tunamatumaini atatekeleza ahadi zake kwa asimilia zaidi ya 90, katika ahadi zake aliahidi kufufua viwanda , katika kufufua viwanda asisahau zao la mkonge ,zao hili kwa sasa limekuwa na soko kubwa sana ukilinganisha na kipindi cha nyuma mkonge kwa sasa grade ya SS kwa tani 1 ni takribani US dollar 2500- 3000 katika soko la dunia na local market ni makadirio ya Tsh 2,500,000 kwa tani , na SSUG ni takribani US dollar 1900-2200 kwa tani
Hivyo basi katika mashamba ya mkonge ajira nyingi zinaweza zalishwa na vijana wengi kuajiriwa wasomi na wasio wasomi na kulipwa vizuri , mashamba mengi yamebinafsishwa kwa wawekezaji ambao wanapunja maslahi ya wafanyakazi hasa unskilled labor kwa kuwapa ujira wa 4950 kwa siku ambayo ni ndogo kulinganisha na kinachozalishwa pia chama cha wafanyakazi mashambani TPAWU wakupe ushirikiano kurekebisha mishahara ya mashambani itakayokidhi maisha ya sasa
Mashamba mengi yamekufa na machache yanauhai , hivyo juhudi zifanyike kurudisha zao la mkonge katika ubora na kupunguza tatizo la ajira kwani mahitaji kwa mkonge duniani ni makubwa sana kulipo hapo awali
Nawasilisha, nikiwa nimefanya research ya kutosha kuhusu zao la mkonge TanzaniaPamoja na kwamba sina imani na chama chako, ila naomba unishawishi wewe binafsi katika serikali yako.
Kama ulivyojinaji kuwa serikali yako, yani Tanzania ya Magufuli itakuwa KAZI TU, basi naomba udhihirishe hivyo katika baraza lako la mawaziri.
Kabla hata sijataka kujua waziri mkuu ambaye ataendana na sura ya kauli mbiu yako, lakini nataka usituletee watu hawa ambao walikuwa mzigo kwa taifa na waliolifikisha nchi hapa ilipo chini ya aliyekutangulia pamoja na waziri mkuu wake.
1. Sopteter Muhongo.
Huyu pamoja na kwamba tunaambiwa hakuhusika moja kwa moja kwenye kashfa xa escrow lakini alikuwa kinara wa utetezi katika sakata hili. Pia ni miongoni mwa waziri wenye elimu kubwa lkn hakuwa na mkakati bunifu wa kutatua tatizo la umeme nchini zaidi ya kuiacha tanesco kwenye deni kubwa. Pia ni miongoni mwa viongozi ambao hawathamini wawekezaji wa ndani, anaamini nchi itajengwa na wazungu au wachina.
2. Lazaro Nyalandu.
Huyu ni miongoni mwa mawaziri ambao tumeshuhudia tembo wakiuliwa kwa wingi, na twiga wetu wakisafirishwa kwenda nje, hafai katika serikali yako, kwani atafanya kazi ya mazoeaa ya serikali ya awamu ya 4.
3. Mwigulu Nchemba.
Pamoja na kwamba hakukaa kwenye wizara ya fedha kwa mda mrefu, lkn ni miongoni mwa vijana ambao hawana adabu katika taifa hili. Ni mmoja wa wanasiasa wachanga ambao hajali matamshi yake mbele ya umma, haangalii baada ya hapa athari zake zitanipeleka wapi, sio mstaarabu.
4. Willium Lukuvi.
Huyu kwa mwendo wa kasi inayohitajika nchini hatufai, utendaji wake hauto tofautiana na wa awamu ya 4, hana jipya ndani ya serikali yako.
5. Shukuru Kawambwa
Huyu ni moja ya mawaziri walioshusha thamani ya elimu yetu. Sio mbunifu. Fedha za fidia za rada mpaka leo hatujui matumizi yake yalienda wapi, hatufai kabisaa.
6.Hawa Ghasia.
Huyu mama bado uchama umemkaa kichwani kuliko maslai ya taifa. Hayupo active katika utendaji wake.
7. Jumanne Maghembe.
Huyu ni moja ya mawaziri ambao ndio chanzo cha huduma mbovu za elimu na maji. Elimu yake ni kubwa lkn haina msaada kwetu.
8.Harrison Mwakyembe.
Huyu kinachompa sifa ni lile sakata la richmond ambalo tunamwona kama shujaa. Lakini kiukweli hafai hata kuwa mwenyekiti wa kijiji. Sijaona mafanikio yake katika wizara alizozisimamia, ni mzigo ana asili ya mtandao ambao ni chanzo cha utendaji mbovu nchini. Ni mafya wa kisiasa
9. Magreth Sitta
Mama huyu tangu zama ni outdated, haendani na kasi ya dunia, yupo nyuma na mda, hafai katika serikali yako.
10. Sofia Simba
Hana tofauti na Mama sitta, tena huyu uchama na mtandao wa uongozi umemjaa kichwani, hafai katika serikali yako.
11. Andwer Chenge
Najua huyu unamfahamu vema
12. Anna Tibaijuka
Najua unamfahamu vizur
13. Willium Ngeleja
Najua wamfahamu vzr
NB.
1. Mheshimiwa Rais kuna vijana wengi ambao naamini katika utendaji wao lkn siamini kundi lake, na mmoja wao ni Januari Makamba. Huyu binafsi namwamini kiutendaji, ubunifu lakini kinachomsumbua ni kutaka madaraka makubwa, kundi lake lililo nyuma yake, Huyu badala ya kuchapa kazi atakuwa anawaza urais baada yako kustaafu. Kwa mtazamo wangu ungemweka kando kwa mda baada ya miaka miwili ndo uumpe majukumu.
2. Kwa kukusaidia mh Rais ni vema ukachagua mawaziri wachache ambao wengi wao hawakuwa mawaziri, sio viongozi katika chama, vijana, wenye elimu isiyo na shaka. Hawa ndio wataileta tanzania mpya ya HAPA KAZI TU.
Mh Rais ukikosea kwenye baraza la mawaziri basi jua umeuwa nchi, na hapo tutadhibitisha kuwa hakuna cha Magufuli 4 change itakuwa ccm ni ile ile.
Asantee.Hali ya Kisiasa
1. Mgogoro wa Zanzibar ni jukumu lako kwa sasa halikwepeki. Tafuta wasuluhishi wawili (kutoka Bara na Visiwani) wakusaidie kulishughulikia hili
2. Katiba mpya ya JMT ? pengine si ajenda ya chama chako kwa sasa lakini linahitaji dhamira yako ? chonde chonde litendee haki taifa hili
Mfumo na Uendeshaji wa Serikali
3. Uza mashangingi ya Serikali na ubakize machache tu kwa shughuli muhimu. Watumishi wa Serikali wakopeshwe magari na wapewe mafuta ili kuokoa fedha nyingi mno zinazopotea kiholela.
4. Rejesha nyumba za Serikali kwani wananchi wengi hatuna imani kuhusu dhamira, mantiki na umuhimu wa kuziuza nyumba za Serikali
5. Punguza sana idadi ya Wizara na Mawaziri ili kupunguza gharama
6. Boresha kipato cha Watumishi serikalini ili kuwaongezea morali
7. Toa fursa katika vipindi tofauti mikoani ukutane na wananchi wenye matatizo uwasikilize ana kwa ana, mmoja mmoja (uwe rais wa wananchi)
8. Misamaha ya kodi ni donda ndugu linalohujumu Taifa mapato, dhibiti hili kwa nguvu zako zote.
9. Panua wigo wa vyanzo vya mapato ya Serikali ? hili ni muhimu sana
10. Dhibiti safari za nje zisizo za lazima kwa Viongozi waandamizi wa Serikali
Rushwa na Ufisadi
11. Mahakama ya Rushwa na Ufisadi ianzishwe kama ulivyoahidi
12. TAKUKURU ipewe mamlaka ya kuwafikisha watuhumiwa mahakamani bila kibali cha DPP
Afya, Maji na Mazingira
13. Karabati hospitali za umma (Taifa, Mikoa, Wilaya) ziko katika hali mbaya (Zahanati kwa kila kijiji inawezekana!)
14. Imarisha Hospitali ya Muhimbili ikidhi viwango vya kimataifa ili kupunguza gharama za matibabu nje ya nchi
15. Panua wigo wa Mfuko wa Bima ya Afya ili ijumuishe wananchi wote (Rwanda wameweza hili) watakaochangia kiwango nafuu
16. Miji na Majiji ni machafu mno (taka ngumu na maji taka), imeshindikana kubadili hali na inaelekea hakuna suluhisho, inabidi tuzoe uchafu ?tunaomba wahusika wageuke taka
17. Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto iboreshwe kwa nguvu zote
18. Serikal igharimie magonjwa hatarishi ikiwemo saratani na UKIMWI
19. Matumizi ya mifuko ya plastiki yapigwe marufuku (Rwanda, Zanzibar imewezekana)
20. Anzisha Mfuko wa Maji Vijijini ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa maji katika maeneo yote
Elimu
21. Wanafuzi wengi wa elimu ya juu hawakupata mikopo kwa mwaka2015/2016? litatue hili kwani ni aibu
22. Elimu ya bure hadi kidato cha nne iwe kweli na yenye ubora
23. Shule ziimarishwe kwa kupatiwa madarasa, maabara, vitabu, walimu na lishe muafaka
24. ?One Computer, One Pupil? ? tujenge taifa la kisasa na linaloendana na mabadiliko ya nyakati kimaendeleo
25. Anzisha Kamisheni ya Taifa ya Ushauri kuhusu elimu
Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Viwanda
26. Fufua kilimo cha mazao asilia (mkonge, kahawa)
27. Anzisha Mfuko wa Taifa wa Kilimona Mifugo utakaotoa mikopo kwa wakulima, wafugaji na wavuvi
28. Imarisha na jenga miradi ya umwagiliaji na majosho ya mifugo
29. Imarisha vyama vya ushirika na viwezeshe kujitafutia masoko
30. Futa kodi zote kandamizi kwa wakulima, wafugaji na wavuvi
31. Anzisha viwanda vya kusindika mazao ya kilimo, ufugaji na uvuvi
32. Weka kodi nafuu na shindani kuhamasisha wawekezaji
Miundombinu na Uchukuzi
33. Punguza gharama za vifaa vya ujenzi ili wananchi wengi wamudu kujenga nyumba bora
34. Fufua Shirika la Ndege la Taifa (ATC)
35. Imarisha miundombinu ili kuondosha misongamano katika majiji na miji mikubwa (Dar, Mwanza, Mbeya, Arusha)
- Usikubali kofia mbili; wewe ni Raisi, uenyekiti wa CCM muachie mwingine ili chama kibaki chama na serikali ibaki serikali.
- Washauri Wabunge wa CCM, watangulize maslahi ya taifa mbele ya maslahi ya chama.
- Washauri Wabunge wa CCM kama itawezekana wamchague Spika wa Bunge asiyeegemea upande wowote.
- Pokea ushauri kutoka kwa vyama vya siasa lakini uwe huru kufanya maamuzi kulingana na matakwa ya Katiba ukizingatia maslahi ya wananchi.
- Usiruhusu Ikulu kutumika kwa maslahi ya CCM, vikao vya chama vifanyike nje ya Ikulu.
- Washauri CCM waachie mali za wananchi kwa kuzirudisha mikononi mwa wananchi kupitia serikali.
- Agiza vyombo vya dola vitoe haki sawa kwa wananchi bila upendeleo.
- Futa sheria zote kandamizi zinazozuia uhuru wa kutafuta, kupokea na kutoa habari. Vyombo vyote vya habari viwe huru.
- Hakikisha mikataba yote tunayoingia inawekwa wazi ili vijadiliwe na kupitishwa na Bunge.
- Vikumbushe vyombo vya dola kwamba jukumu lao la kwanza ni kuwalinda Watanzania na mali zao na si kupambana nao.
Watu wengi wanaishi wilayani na mahitaji yao mengi yanatatuliwa wilayani hukohuko, hivyo kuweka watendaji mahili na wabunifu kwenye ngazi ya wilaya ndio mtihani wa kwanza wa rais Magufuli. Wakuu wa wilaya na watendaji wengine wa JK sio kabisa, na huwenda ndio chanzo cha migogoro mingi ya wananchi dhidi ya serikali yao. JPM hana namna nyingine zaidi ya kuwaweka pembeni watendaji wote wavivu na wabadhilifu wilayani na mikoani ambao wengi wao wameshachukiwa tayari na wananchi wao.
Mtihani wa pili ni namna atakavyo atakavyotumia uwezo wake kupambana wa watu wajanjawajanja kama vile akina Lyatonga, Chenge, Tibaijuka, Manji, Aziz, Nazir, Harison, Samuel na wengine. Kwa muonekano wao ni wapenda sifa binafsi na kujali maslahi yao tu.
Mtihani wa tatu ni namna atakavyoweza kukaa mbali na kundi la mzee Mkapa waliohusika na kuuza viwanda, migodi, mabenki, mashamba, nyumba za serikali na hata waliotajwa kwenye kashifa ya EPA, meremeta, rada, ndege ya rais, n.k, ambao ni chanzo kikubwa leo cha ukosefu wa ajira kwa vijana na ongezeko kubwa la deni la taifa.
Mtihani wa Nne ni namna ya atakavyopambana na wimbi la watoto na wajukuu wa viongozi wa wakuu wa CCM wanaotaka kupewa nafasi serikalini kwa upendeleo kutumia nafasi za wazazi wao.
Mtihani wa Tano ni namna atakavyoweza kupambana na udini, ukabila, na ukanda katika kutoa nafasi za ajira nchini. Hali ilivyo hivi sasa ni mbaya sana, ajira wizarani, kwenye vitengo mbalimbali, mialiko kwenye mikutano, semina na nafasi za mafunzo inatolewa kwa ukanda, ukabila, udugu na udini.
Asipozingatia haya atahesabika kuwa ameanza na mguu mbaya sana utakaomgarimu sana uchaguzi wa 2020.Secta ya bunge kitengo cha huduma na haki za mbunge kilichokuwa chini ya Chenge kilipangia bunge masulufu makubwa mno na bado wabunge kwa makusudi au kwa utovu wa adabu walikuwa wanaona haziwatoshi.
Mfano posho za kuhudhuria bunge ni shs 300.000 bado wabunge walikuwa wanaona hazitoshi ziongezwe chini ya Chenge
Mh. Rais kubana matumizi ya serikali iangalie sana secta hii ya bunge
Pia ninakuomba usitishe mikopo ya mashangingi, waheshimiwa wabunge wanunue RAV 4 au NOA kwa hela zao kwa sababu majimbo yamegawanywa na kuwa madogo yanayoweza kufikika kilaisi na usafiri huo.
Mh Rais fanya kazi ya ubunge iwe ngumu lli uchaguzi ujao wanachi wasiikimbilie
Ushauri huu pia nimekutumia kwa e.mail tafadhari naomba unijibu kama kutakuwa na ugumu katika utekelezaji wake
KIFUPI: Bunge linamega sehemu kubwa sana ya keki ya Taifa, serikali ya awamu ya tano liipunguze keki hiyo.
No comments :
Post a Comment