Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, November 5, 2015

Mawaziri wa JK watakiwa kurudisha magari Ikulu

Maegesho ya magari ya Mawaziri bungeni Dodoma. 
By Fidelis Butahe, Mwananchi
Dar es Salaam. Mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Nne wametakiwa kurejesha Ikulu magari wanayotumia mara baada ya kuapishwa Rais Mteule John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru leo.
Mawaziri hao wamekuwa wakiyatumia magari hayo tangu Bunge la Muungano lilipovunjwa, huku baadhi wakiwa wameshapoteza nafasi ya kurudi bungeni baada ya kushindwa kwenye majimbo yao na wengine kuanguka kwenye kura za maoni.
Jana, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema katika taarifa yake kuwa mara baada ya kumalizika kwa sherehe za kumuapisha Dk Magufuli, magari hayo yatabandikwa kibao cha namba za ST na madereva kuwarejesha nyumbani mawaziri waliokuwa wakiyatumia na baadaye kuyapeleka Ikulu kusubiri kupangiwa kazi nyingine.
Agizo hilo linawahusu mawaziri wote wa Serikali ya Awamu ya Nne, isipokuwa aliyekuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga ambaye tayari alisharejesha gari hilo baada ya kuamua kuhama CCM, hivyo kupoteza sifa za kuendelea kuwa waziri.
Wengine ni aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi), Celina Kombani ambao walifariki dunia hivi karibuni.
“Utaratibu uko wazi miaka yote,” alisema Balozi Sefue. “Waziri anabaki kuwa waziri mpaka siku na muda Rais mpya anapoapishwa.
“Pale kiwanjani (uwanja wa uhuru) wakati bendera ya Rais wa Awamu ya Nne inashuka, na wale mawaziri ndiyo unakuwa mwisho wao. Kuanzia hapo hawaruhusiwi kutumia magari hayo na yanatakiwa kurudi Ikulu kufanyiwa matengenezo na kusubiri mawaziri wengine.”
Balozi Sefue alisema Serikali haina utaratibu wa kununua magari mapya na kwamba magari yanayotumiwa sasa yangeweza kubaki wizarani na kutumiwa na makatibu wakuu, lakini utaratibu ulibadilika ili kubana matumizi.
“Kwa hiyo yatarejeshwa kwa ajili ya kutumiwa na mawaziri wengine,” alisema.
Alisema wakati Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa akimuachia kijiti Rais Kikwete, utaratibu wa kurejesha magari uliotumika ni huohuo.
Alipoulizwa kama utaratibu huo ulikuwa ukitumia nyuma ya hapo alisema ulitumika mwaka 2005, lakni hana kumbukumbu ya kabla ya hapo.

No comments :

Post a Comment