Akizungumza na Nipashe mjini Zanzibar jana, mwanasheria huyo alisema wanaosema Dk. Shein amefikisha ukomo wa kubakia madarakani wanatafsiri kifungu cha 28 (2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kwa utashi wa kisiasa.
Alisema kwa mujibu wa kifungu cha 28(1) (2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Dk Shein bado anaendelea kuwa Rais mpaka hapo Rais anayefuata ale kiapo cha kuwa Rais baada ya kutangazwa na Tume ya Uchaguzi visiwani humo (Zec).
“Mahakama kazi yake ni kutafsiri sheria, kama kuna mtu anapinga Dk. Shein kuendelea kubakia madarakani basi akafungue kesi ya katiba mahakamani, lakini tusitafute umarufu kwa jambo ambalo lipo wazi kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar,” alisema na kuongeza:
“Katika kutafsri katiba au sheria kigungu cha 28 (1) ndicho kinapaswa kufuatwa ambacho kinaeleza wazi kuwa: ‘Kufutana na Katiba hii mtu ataendelea kuwa Rais mpaka Rais anayefuta ale kiapo cha kuwa Rais’.”
“Katika kutafsri katiba au sheria kigungu cha 28 (1) ndicho kinapaswa kufuatwa ambacho kinaeleza wazi kuwa: ‘Kufutana na Katiba hii mtu ataendelea kuwa Rais mpaka Rais anayefuta ale kiapo cha kuwa Rais’.”
Mwanasheria Mkuu huyo wa zamani wa Zanzibar, alisema wananchi wamekuwa wakiyumbishwa katika suala hilo na wanasheria ambao wamekuwa wakitafsiri kifungu cha 28 (2) kwa utashi wao wa kisiasa, kwani kifungu cha kwanza cha 28 (1) ndiyo kinachopaswa kuzingatiwa badala ya kifungu kidogo cha 28 (2) katika tafsiri ya sheria.
“Kama kweli amefikia ukomo wa uongozi mbona Makamu wa Kwanza wa Rais na Mawaziri wa Cuf bado wanaendelea na nyadhifa zao?,” alihoji mwanasheria huyo.
Alisema Rais kukaa madarakani zaidi ya muda wake siyo jambo geni, kwani hata Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin Mkapa, aliongeza muda baada ya kufariki aliyekuwa Mgombea Mwenza wa Chadema, Jumbe Rajabu Jumbe, wakati taifa likiwa katika matayarisho ya uchaguzi mkuu mwaka 2005.
“Sitaki umaarufu, tafsiri ya serikali ipo sahihi na Dk. Shein yupo kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, kama kuna mtu anapinga basi aende mahakamani, tusiwapasue vichwa bure wananchi,” alisema.
Hata hivyo, Mbwezeren alisema kwamba Zec inapaswa kukaa pamoja na wadau wake wote kuwasikiliza wakiwamo wanaodai uchaguzi umevurugwa na wale wanaotetea ulikuwa huru na wa haki ili kuwekana sawa mambo yasonge mbele.
Mjadala juu ya Rais Dk. Shein kufikisha ukomo Novemba 2, mwaka huu ulinza kuzungumzwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad na Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS), Awadhi Ali Said, pamoja na mgombea wa urais wa AFP, Soud Said Soud ambao wamemtaka kuachia madaraka hayo.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment