Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, November 11, 2015

NYANZA: ATE yataka ‘Hapa Kazi Tu’ hadi sekta binafsi

Rais John Magufuli akisalimiana na baadhi ya wagonjwa waliolazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alipofanya ziara ya ghafla hospitalini hapo Novemba 9, 2015. Picha ya Maktaba
By Mwandishi yetu, Mwananchi
Mwanza. Chama cha Waajiri TAnzania (ATE) kimesema kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ inatakiwa kuwafikia wafanyakazi wa sekta binafsi badala ya watumishi wa umma pekee ili wabadike na kuleta maendeleo nchini.
Kauli mbiu hiyo imekuwa ikitumiwa na  Rais John Magufuli wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka huu, hata baada ya kuchaguliwa, kuapishwa na kuanza kuwatumia Watanzania akiwa Ikulu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Dk Aggrey Mlimuka alitoa rai hiyo wakati akizungumza na wanachama wa chama hicho  jijini Mwanza mwishoni mwa wiki iliyopita.
Alisema mapendekezo mengi ya waajiri yanasubiri utekelezaji kwani tayari yamewasilishwa serikalini. “Mfano, saa za kazi ni 45 kwa wiki, ambazo ni ndogo. Pia kuna utovu wa nidhamu kazini  na upendeleo kwa mfanyakazi anayemwibia mwajiri.  Sheria ya Kazi na Uhusiano Kazini imekuwa ya kibaguzi,” alisema na kuongeza kuwa:
“Sekta binafsi tunaambiwa tumlipe mfanyakazi mshahara wake wote wakati kesi ikiendelea, lakini mtumishi wa Serikali analipwa nusu mshahara.”
Alisema sheria ipo kimya kuhusu muda wa ukomo kwa mfanyakazi anayejifungua,.
“ Sheria inasema atapewa saa mbili za kunyonyesha, hivyo anaweza kuchelewa kazini au kuondoka mapema, tunahitaji ukomo, kama ni miezi sita sawa,” alisema.
Kuhusu Sheria ya Fidia, Dk Mlimuka alisema ni ya kibaguzi  kwani watumishi wa Serikali wanalipiwa asilimia 0.5 ya mshahara wao, lakini sekta binafsi waajiri wanatakiwa kulipa asilimia moja.
“Kuna kampuni ambazo zimeweka bima kulipa wafanyakazi wao wanapopata majanga, hawa wameongezewa gharama hivi sasa watalazimika kulipa maradufu tunahitaji Rais Magufuli kuangalia masuala haya,” alisema.
Alisema wanaomba kupunguziwa tozo ya ufundi stadi ambayo ni asilimia tano ya mishahara ya wafanyakazi. “Tunaomba Rais atoe fursa kukutana na waajiri kama ilivyo wafanyakazi,” alisema.
Mratibu Mradi wa ATE, Joyce Nangai alisema kufunguliwa kwa ofisi zao zitakazohudumia mikoa ya Kanda ya Ziwa, itasaidia kuwa karibu na wanachama wao.

No comments :

Post a Comment