Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, November 2, 2015

TAARIFA YA CUF KWA VYOMBO VYA HABARI NCHINI!



Kufuatia taarifa iliyotolewa na Ikulu Dar es Salaam, na pamoja na jitihada za awali za Makamu wa Kwanza wa Rais na Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kujaribu kuwasiliana na Rais Jakaya Kikwete kwa njia ya simu, leo hii Maalim Seif amemuandikia barua rasmi kumuomba wakutane ili kuzungumzia hali ya kisiasa ya Zanzibar kufuatia uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015.

Kwa upande mwengine, kufuatia maelekezo ya Rais Kikwete, CUF imekubali kufanya mawasiliano na wasaidizi wa Rais ili kupanga utaratibu wa kukutana na Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jenerali Davis Mwamunyange, ili kuzungumzia hali ya usalama ya Zanzibar kufuatia uchaguzi mkuu huo wa tarehe25 Oktoba, 2015.

Katika hatua nyengine, leo Maalim Seif Sharif Hamad alikutana na viongozi wa dini ya Kiislamu na Kikristo wa hapa Zanzibar kuzungumzia suala zima la uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba na kuwaomba viongozi hao kuingilia kati suala hili ili kuhakikisha nchi inabaki katika hali ya amani na utulivu na pia kuhakikisha maamuzi ya Wazanzibari waliyoyafanya kupitia uchaguzi huo yanaheshimiwa.

Tunapenda kuwahakikishia kuwa tutachukua kila juhudi zilizomo kwenye uwezo wetu katika kuupatia ufumbuzi mgogoro uliojitokeza na kufanya kazi na kila aliye tayari kushirikiana na sisi katika kutunza amani ya nchi yetu na kuilinda demokrasia yetu.

HAKI SAWA KWA WOTE
ISMAIL JUSSA
MKURUGENZI WA MAWASILIANO – CUF

//FB Salma Said

No comments :

Post a Comment