Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, November 11, 2015

Tunaridhishwa mazungumzo ya kutatua mgogoro Z'bar - EU.

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein.
Umoja wa Ulaya (EU) umesema unaridhishwa na mazungumzo yanayoendelea sasa katika kutatua mgogoro wa kisiasa Zanzibar na kwamba wana imani utamalizwa kwa mazungumzo yenye amani kwa maslahi ya wananchi.
 
Kadhalika, imeipongeza Tanzania kuwa miongoni mwa nchi yenye amani na kufuata demokrasia barani Afrika katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu.
 
Hayo yalielezwa na Balozi wa EU nchini Tanzania, Filiberto Sebregondi, wakati wa maadhimisho ya miaka 40 ya ushirikiano baina ya Tanzania na EU yaliyoanza mwaka 1975.
 
Kauli hizo zimetolewa ikiwa ni siku mbili zimepita baada ya Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, kukutana kwa kuzungumza kwa saa sita na nusu na mgombea mwezake wa urais kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, kujadili mgogoro wa uchaguzi, baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec), Jecha Salim Jecha, kufuta matokeo.
 
Mazungumzo hayo ya kutafuta muafaka Zanzibar, pia yalihudhuriwa na Rais mstaafu  Ali Hassan Mwinyi na Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu ya Zanzibar na ajenda kubwa ilihusu mgogoro wa uchaguzi visiwani humo.
Sebregondi alisema  EU ina imani kubwa na mazungumzo hayo yanayoendelea ya kutafuta amani visiwani humo kuwa yataendelea kwa mazungumzo yenye amani na kuleta muafaka.
 
Alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoheshimu demokrasia barani Afrika hususan katika masuala ya uchaguzi kwa amani na upendo.
 
Aidha, alisema katika miaka 40 ya ushirikiano, EU imetoa zaidi ya Euro bilioni tatu (Sawa na Sh. trilioni 6.8) zilizotumika katika ujenzi wa miundombinu hususan vijijini, kusaidia elimu, miundombinu ya maji, jamii katika kuimarisha utawala bora na haki za binadamu, masuala ya bajeti na juhudi za kutokomeza umaskini, ujinga na maradhi.
 
Katika maadhimisho hayo, EU ilizindua kitabu kiitwacho ‘Partnership in Action’ kinachoelezea mafanikio na ushirikiano baina ya EU na Tanzania katika kipindi cha miaka 40.
 
Naye Katibu mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile alisema EU wamekuwa na msaada mkubwa kwa Tanzania tangu mwaka 1975 na kueleza kuwa tangu mwaka 2014 hadi 2015, EU imeshatoa Euro milioni 620 (sawa na Sh. bilioni 1.4).
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment