Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, November 4, 2015

Wasanii wawataka Wazanzibari watulie!

TAFUTA YA AT, baby-J
WASANII mbalimbali waliopo visiwani Zanzibar wameonyesha kuguswa na hali ya Zanzibar, huku wakiwataka mashabiki wao wanaoishi visiwani humo wawe watulivu kipindi hiki cha mgogoro wa kisiasa visiwani humo.

Wasanii hao waliliambia MTANZANIA kwa nyakati tofauti kwamba wameguswa na mgogoro huo, hivyo mashabiki wao hawatakiwi kuwa na papara kwa kuwa mgogoro huo unafanyiwa kazi na utapatiwa ufumbuzi.

Msanii Ally Ramadhan ‘AT’ alisema nchi nyingi huwa zinaingia kwenye machafuko kipindi cha uchaguzi, lakini Zanzibar ni tofauti kwa kuwa viongozi wameshafanya jitihada za kutatua mgogoro huo.

“Kwetu Zanzibar tunasifika kwa utu, ukarimu na ubinadamu, hivyo ili dunia ijue kuwa sisi siyo watu wa fujo, nawasihi wananchi wenzangu tuwe watulivu na tuache mamlaka husika wamalize mgogoro huu kwa amani ili tuendelee na shughuli zetu kama kawaida,” alisema AT.

Wasanii wengine waliowaasa mashabiki wao wawe watulivu ni Jamila Abdallah ‘Baby Jay’ na Rico Single.

/Mtanzania.

No comments :

Post a Comment