Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, December 11, 2015

Magufuli amponza Waziri Mkuu Uingereza


Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron
Kitendo cha Rais Dk. John Magufuli, kushiriki kwenye shughuli ya usafi juzi kama sehemu ya kusherehekea kumbukumbu ya Siku ya Uhuru inayoadhimishwa kila mwaka Desemba 9, imemponza Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron.
 
 Katika toleo lake la jana, gazeti la The Telegraph la nchini Uingereza, pamoja na kusifu kitendo hicho cha Rais Magufuli, lilihoji iwapo Cameron anaweza kushiriki kufanya usafi kwenye mitaa ya jiji hilo kama alivyofanya Rais Magufuli. Likiwa limetoa picha zake mbalimbali zilizokuwa zikimuonyesha akishiriki kwenye operesheni ya usafi nje ya Ikulu, gazeti hilo lilisema kwamba Rais Magufuli aliungana katika shughuli hiyo na wavuvi kutoka Soko la Feri jijini Dar es Salaam, kuokota uchafu na kupakia kwenye gari la kubeba taka na kwenda kutupa kwenye dampo. Liliendelea kuandika kwamba Dk.  Magufuli aliyeingia madarakani Novemba, mwaka huu, alifuta sherehe za siku ya kumbukumbu ya Uhuru na badala yake akaagiza siku hiyo itumike kwa kufanya usafi pamoja na mambo mengine, kwa ajili ya usalama wa afya zao.
 
Maelfu ya watu nchini kote walijitokeza juzi kushiriki kwenye shughuli hiyo ya usafi iliyokuwa maalum kwa ajili ya kudhibiti ugonjwa wa kipindupindu.Gazeti hilo la Telegraph linakuja na habari hiyo ikiwa ni muda mfupi baada ya mwandishi mwingine nchini Nigeria, kuandika akimtaka Rais wa nchi yake, Muhammadu Buhari, kuiga baadhi ya mambo anayofanya Rais Magufuli wa Tanzania ili ayatumie kwenye uongozi wake.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment