By Salma Said na Haji Mtumwa, Mwananchi
Zanzibar. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema mfumuko wa bei za vyakula umefikia asilimia 10 katika Visiwa vya Unguja Pemba.
Sababu zinazoelezwa kusababisha mfumuko huo ni wafanyabiashara kutoingiza bidhaa kutoka nje ya Zanzibar. Meneja Msaidizi Idara ya Uchumi, Dk Maduhu Kazi alisema ongezeko la bei za bidhaa linazikumba nchi nyingi za Afrika.
Mkuu wa kitengo cha takwimu za bei Zanzibar, Khamis Hamad Shauri akisoma ripoti ya mfumuko wa bei wa Novemba, alisema miongoni mwa sababu kuu zinazosababisha kupanda kwa bei ni ukosefu wa bidhaa katika masoko makuu ya biashara.
No comments :
Post a Comment