Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya fani ya Mazingira wakiwa katika sherehe za mahafali ya kumaliza mafunzo yao hapo kwenye Kampasi ya chuo Hicho Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Wahitimu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya fani ya maabara wakifuatilia matukio mbali mbal;I yaliyokuwa yakiendelea kwenye mahafali ya kumaliza mafunzo yao hapo Mbweni.
Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya fani ya Uuguzi wakisubiri kuhudhurishwa baada ya kumaliza mafunzo yao ya miaka Mitatu katika chuo cha Taaluma za Sayanasi za Afya Mbweni.
Wahitimu wa Fani ya Uuguzi wakila Kiapo baada ya kumaliza mafunzo yao ili kwenda kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili na kanuni za utumishi Serikalini.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Mbweni Dr. Abdulla Ismail Kanduru kushoto akiteta na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyemuwakilisha Rais wa Zanzibar kwenye mahafali ya 22 ya Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Mbweni.
Balozi Seif akimkabidhi Cheti Maalum Asha Issa Juma wa Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya akiwa Mhitimu bora wa Fani ya Afya Kinywa na Meno mwaka 2015.
Balozi Seif akimkabidhi Cheti Maalum Salama Witi Asfau wa Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya akiwa Mhitimu bora wa Fani ya Usanifu wa Vifaa Tiba vya Hospitali kwa mwaka 2015.
Balozi Seif kwa niaba ya Rais wa Zanzibar akizungumza wakati akiwahutubia wahitimu wa Mahafali ya 22 ya Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Kulia ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Zanzibar Dr. Abdullah Ismail Kanduru.
Mkuu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Zanzibar kutoka Kushoto Dr. Haji Mwita Haji akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Zanzibar Dr. Abdullah Ismail Kanduru wakifuatilia matukio mbali mbali yaliyojiri kwenye mahafali ya chuo hicho mkupuo wa 22.
Picha na –OMPR –ZNZ.
No comments :
Post a Comment