TAA pia kimesema nidhamu ya matumizi na ukusanyaji mapato ni nguzo kuu ya maendeleo ya nchi yoyote na hata kwa kampuni na familia kwa ujumla. Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa TAA, Fred Msemwa, wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano ya kuwabana wasiolipa kodi chini ya Rais Dk. John Magufuli.
“Tunampongeza Rais John Magufuli kwa hatua mbalimbali alizozichukua na anazoendelea kuzichukua katika suala zima la ukusanyaji mapato, kubana matumizi na kuleta nidhamu ya fedha,” alisema Msemwa. Alisema kwa kipindi kifupi ambacho ameingia madarakani, Rais Magufuli ameweza kukusanya kiasi cha zaidi ya Sh. trilioni moja na kwamba juhudi hizo ni za kuungwa mkono na Watanzania wote.
“Rais amewafundisha Watanzania na kuwaonyesha kuwa nchi hii ina rasilimali nyingi na vyanzo vingi ambavyo vinaweza kuiongezea mapato na kisha kuachana na kuomba msaada usio wa lazima,” alisema na kuendelea:
“Hatuamini kwamba aliyekuwapo madarakani hakusimamia mapato kama mwenzake, bali ni kitendo cha muda mfupi wa kuwapo madarakani na kuweza kukusanya mapato kama hayo, ndicho tunachozungumzia.”
“Hatuamini kwamba aliyekuwapo madarakani hakusimamia mapato kama mwenzake, bali ni kitendo cha muda mfupi wa kuwapo madarakani na kuweza kukusanya mapato kama hayo, ndicho tunachozungumzia.”
Alisema mapato ambayo Rais Magufuli ameyakusanya kwa kubana matumizi tangu alipoingia madarakani ni Sh. bilioni nne, ambazo zingetumika katika Sherehe za Uhuru.
Msemwa alisema fedha hizo zimeelekezwa katika ujenzi wa barabara ya Bagamoyo kutoka Morocco hadi Mwenge jijini Dar es Salaam, huku Sh. milioni 200 za kupongeza wabunge zikiwa zimeelekezwa kwenye ununuaji wa vifaa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mbali na hizo, Sh. milioni 20 za Siku ya Ukimwi duniani ambazo kitaifa zilipangwa kufanyika mkoani Singida, zilitumika kwenye shughuli nyingine muhimu za kijamii. Msemwa alisema Rais Magufuli pia aliweza kuzuia semina elekezi kwa mawaziri na kuokoa zaidi ya Sh. billioni mbili, huku zaidi ya Sh. billioni 10.5 za ukwepaji kodi kupitia makontena zikiwa zimeshakusanywa na TRA.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment