Shirika la Umeme (Tanesco) makao makuu
Kwa ufupi
Moshi. Shirika la Umeme (Tanesco) wilayani Mwanga limepata hasara ya zaidi ya Sh151.2 milioni kwa kipindi cha miezi miwili kutokana na uharibifu wa miundombinu ya nishati hiyo.
Alisema mita 2,645 zimeibwa na kusababisha shirika hilo kupata hasara na kushindwa kutoa huduma bora kwa wateja.
Mkuu wa wilaya, Shahib Ndemanga alisema hatawavumilia wala kuwafumbia macho watu watakaogundulika kujihusisha na wizi wa nyaya na nguzo za umeme.Ndemanga alisema kwa kipindi alichofika wilayani hapo matukio hayo yamekuwa yakiongezeka ukilinganisha na miaka ya nyuma.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani alisema wanashikilia watu 28 wanaotuhumiwa kuhusika na wizi wa nyaya za umeme aina shaba wilayani Mwanga.
Kamanda Ngonyani alisema Desemba 8 walikamata mita 200 za nyaya za umeme zenye thamani ya Sh10.6 milioni na Desemba 9 walikamata mita 300 zenye thamani ya Sh 17.2 milioni.
No comments :
Post a Comment