Naibu mkuu wa Rasilmali Watu wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo Doris Luvanda akipokea Kikombe cha Mshindi wa Mwajiri Bora wa mwaka 2015 kutoka kwa Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa wakati wa kuhitimisha hafla hiyo. Kulia ni Katibu Mkuu Dkt Florens Turuka na Mwenyekiti wa ATE Almas Maige, Mkuu wa Mkoa wa DSM Mhe.Said Meck Sadiki na Mkurugenzi wa ATE Dkt Aggrey Mlimuka.
Dar Es Salaam, Maadili ya kazi yanayoonyeshwa na wafanyakazi wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo Tanzania pamoja na juhudi zinazohitajika katika nyanja ya mawasiliano ya simu ulionyeshwa kuwa mfano katika tuzo mbalimbali zilizonyakuliwa na kampunin ya Tigo Tanzania.
Haya yalijidhihirisha katika sherehe ya kuizawadia kampuni ya Tigo wakati wa sherehe ya mwaka ya utoaji tuzo ya mwajiri bora wa mwaka unaoendeshwana chama cha waajiri Tanzania (ATE) zilizofanyika Ijumaa iliyopita katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Meneja Rasilimali Watu wa kampuni ya Tigo, Doris Luvanda alisema : “tumekuwa tukifanya kazi kwa kasi kadri ambavyo sekta ya rasilimali watu ilivyo kwa sasa na tumehakikisha ya kuwa waajiriwa wetu wamefahamishwa kikamilifu kuhusu bidhaa zetu, na mafunzo ya ndani kila siku yametujengea uimara kwa waajiri wetu
Tigo imefaulu kushinda nafasi za ushindi mbalimbali kama vile Sera ya ujumla ya rasilimali watu na ulinzi, malipo na faida zake.
“Maandalizi ya mashindano yanatayarishwa na mshauri wa kujitegemea anayefanya kazi kuhakikisha ya kuwa chama cha waajiri Tanzania (ATE) kinampata mshindi halali ambaye hujulikana mara tuu baada ya kupitia yale yaliyowasilishwa kwa ajili ya ushindani kukamilika, Mkurugenzi wa ATE, Dr. Aggrey Mlimuka alisema.
Kufuatia mapokezi mazuri ya kila mwaka kwa ajili ya shindano hili la mwaka, kwa mwaka huu jumla ya makampuni 135 zilijaza masuali ya kuandika na baadhi yao 63 zilifanikisha kushiriki kikamilifu katika shindanoahili.
|
No comments :
Post a Comment