Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, December 14, 2015

Walimu watakiwa kuwahamasisha wanafunzi kushiriki michezo

  Walimu walioshiriki mashindano ya michezo mbalimbali wakionyesha vipaji vyao katika mashindano yaliyofanyika viwanja vya nje Amani Mjini Zanzibar Picha na Miza Othman –Maelezo Zanzibar
  Walimu walioshiriki mashindano ya michezo mbalimbali wakionyesha vipaji vyao katika mashindano yaliyofanyika viwanja vya nje Amani Mjini Zanzibar Picha na Miza Othman –Maelezo Zanzibar
 Mkurugenzi  Idara ya Maendeleo ya Michezo, Wizara ya Habari Utamaduni Wasanii na Michezo Tanzania Leonard Tadeo akitowa maeneno ya shukurani baada ya kuwakabidhi  zawadi  washindi  wa  mashindano mbali mbali  ya Walimu kutoka Wilaya 3 Kaskazini, Mjini na Kusini huko katika viwanja vya nje Amani Mjini Zanzibar. Picha na Miza Othman –Maelezo Zanzibar.
 Washindi walioshiriki katika mashindano mbali mbali wakipewa zawadi na Mgezi Rasmini Leonard Tadeo mara baada ya kumaliza mashindano hayo.Picha na Miza Othman –Maelezo Zanzibar.
 Washindi walioshiriki  katika mashindano mbali mbali wakipewa zawadi na Mgezi Rasmini Leonard Tadeo mara baada ya kumaliza mashindano hayo.Picha na Miza Othman –Maelezo Zanzibar.

Na Rahma Khamis/Miza Othman -Maelezo 

Waalimu Nchini wametakiwa kuwapa fursa na kuwahamasisha wanafunzi wa Skuli mbalimbali  kushiriki katika michezo  ili kuwezesha  kupata timu nzuri na kushiriki katika mashindano ya Kimataifa.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari Utamaduni Wasanii na Michezo Tanzania Leonard Tadeo  huko  katika  Uwanja wa Amani nje wakati alipokua akifunga Shamrashamra za  Tamasha siku ya Walimu Duniani.

Amesema katika Nchi ya Tanzania wananchi wengi hulalamika  kwa kutofanya vizuri katika michezo  kutokana na  Waalimu kusahau  wajibu wao wa kuwajenga wanafunzi wao kimichezo tangu wadogo wakati wapo Maskulini jambo ambalo linarejesha nyuma  maendeleo ya michezo hiyo.

Aidha amefahamisha kuwa iwapo jamii itashiriki katika michezo mbalimbali  itaweza kujiepusha na mararadhi sambamba na kujenga afya hivyo zoezi hilo liwe endelevu kwani kufanya hivyo kutasaidia walimu kuwa imara kimichezo.Hata hivyo Mkurugenzi huyo amewataka waalimu kutoa fursa  kwa kushirikiana na Wizara huusika kwenda kusoma katika Chuo cha Maendeleo ya michezo Tanzania Bara ilikuongeza uwezo na idadi y awaalimu wa michzo.

Kwa upande wake mwalimu Mussa  Abdulrabi  kutoka Wizara ya Elimu amesema lengo la kufanya tamasha hiloni kuwafanya walimu kushiriki michezo mbalimbali na kuonesha vipaji vyao  katika michezo hiyo.

Amesema katiaka mwaka huu hakuna changamoto zilizojitokeza hivyo  wanajiandaa mwakani ili wawe na uwezo wa kufanya vizuri zaidi  katika tamasha lijalo .

Sambamba na hayo mwalimu huyo ameaahidi kuwa watawashajiisha walimu wenzao kwenda kujiunga na Chuo cha Maendeleo   ya Michezo ili  kupata walimu wengi  kwa ajili ya michezo kwani Serekali ina nia ya kuendeleza Michezo .

Wakielezea furaha zao washindi katika Tamasha hilo wameiomba Wizara kuangalia suala la michezo zaidi kwa kuandaliwa mafunzo maalum ili kuweza kushiriki katika mashindano  mbalimbali.

Katika shamrashamra hizo kumefanyika michezo ya ikiwemo kuvuta kamba, Mpira wa Mkono,mbio za Gunia pamoja na Mpira wa miguu  kutoka katika Mikoa mitatu ya Zanzibar ikiwemo Mkoa Kusini Unguja , Kaskazini Unguja na Mkoa wa mjini Magharib ambapo Mkoa wa Kaskazini na Mjini ndio walioibuka washindi ikifuatiwa na Mkoa wa Kusini Unguja.

No comments :

Post a Comment