Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, January 6, 2016

Agizo la Makala lazua ‘tafrani’ mitandaoni

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makala
By Daniel Mjema, Mwananchi
Moshi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makala amelalamikiwa na baadhi ya wakazi wa mkoa huo kwa kuruhusu uvunaji wa misitu kwa ajili ya kutengeneza madawati.
Malalamiko hayo yaliendelea kutolewa jana katika mitandao ya kijamii huku wakazi hao wakipinga agizo hilo na wengine wakimtaka afute.
Wakazi hao walidai kuwa agizo hilo litavuruga kazi nzuri iliyofanywa na mtangulizi wake, Leonidas Gama aliyefuta uvunaji wa misitu baada ya mkoa huo kuelekea kuwa jangwa mwaka 2012.
Wiki iliyopita akiwa wilayani Same, Makala aliruhusu uvunaji wa misitu kwa halmashauri ambazo shule zake zina upungufu wa madawati.
Hata hivyo Makala, alipotafutwa jana alisema inavyoonekana agizo lake limepotoshwa kwani hakuagiza uvunaji holela wa misitu, bali utafanyika kwa kibali na usimamizi maalumu.
“Nazionya halmashauri zitakazotumia vibaya vibali hivi. Nilichosema vitatolewa na maofisa misitu baada ya kujiridhisha kuna fursa hizo. Siyo kila mtu ataomba, ni mkurugenzi wa halmashauri,” alisema.
“Sijasema kila mtu atapewa kibali cha kuvuna,” alionya.
Makala alisema tayari ana waraka wa Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), kuhakikisha tatizo la madawati linamalizika katika shule zote nchini ifikapo Juni, mwaka huu.
Hata hivyo, pamoja na ufafanuzi huo, jana ‘hali ya hewa’ ilichafuka na hilo lilithibitishwa na Makala mwenyewe baada ya kusema alipokea simu nyingi za vituo vya redio na wanahabari wakihoji juu ya agizo lake.
Tayari Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) Kanda ya Kaskazini, Cuthberty Mafupa na Mkurugenzi mstaafu wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dk Felician Kilahama wamepinga agizo hilo.   

No comments :

Post a Comment