dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, January 19, 2016

AN OPEN LETTER TO PR. MAGUFULI!


Rais Magufuli tuokoe, tunakufa njaa ujerumani


Mh. Rais wangu Mpendwa Dr. Magufuli,
Pole na majukumu ya kujenga nchi yetu kutokana na changamoto za kujenga nchi yetu. Pamoja na hayo nataka kuchukua fursa hii baada ya uvumilivu wa mda mrefu kukuelezea masikitiko yetu na jinsi tunavyoteseka sisi wananchi wa Tanzania tunaosoma na kuishi hapa Ujerumani. Unaweza ukajiuliza ni kwanini hii barua ya wazi iandikwe kwako na si kwa watendaji walioko chini yako kama waziri wa elimu, katibu mkuu wa wizara, wakurugenzi au makamishina wa elimu. Jibu ni kwamba; HUKO KOTE TUMESHAFIKISHA MALALAMIKO YETU LAKINI HATUKUPATA UFUMBUZI WOWOTE. Lakini pia unaweza ukajiuliza ni kwanini iwe kwa njia ya Jamii Forums? Jibu ni kwamba kama barua, mails, na hata kiongozi wetu kufuatilia malipo yetu toka TCU, HESLB na Wizarani hizo njia hazijazaa matunda na si ajabu ofisi yako haina taarifa hii.

Na kwa msingi huo, mimi nikiwa mmoja wa waathirika na ambaye kwa kiasi kikubwa sana nimefanya jitihada za kila namna ikiwemo kuwasiliana na watendaji wakuu wa TCU, HESLB (Mkurugenzi Mtendaji Mr. , na Mkurugenzi wa Fedha Mr....), na wizara ili kutafuta ufumbuzi wa matatizo yetu, lkn katika njia zote hizo HAKUNA MAFANIKIO NA SASA NI MIEZI MINNE baadhi yetu tunakaa nje ya nchi bila kupata pesa za kujikimu toka Tanzania kupitia HESLB na TCU.

Mh. Rais wangu, sisi waathirika ni wanafunzi tunaosoma huku Ujerumani kupitia mpango maalumu kati ya serikali yetu pendwa na serikali ya Ujerumani kupitia program ya MoEVT - DAAD (ukitaka kujua zaidi kuhusu hii program muulize yule katibu mkuu uliyemuhamisha majuzi kwenda wizara ya sheria kwani anajua kila kitu kuhusu hii programu. Lakini pia waweza kumuuliza yule kamishna wa elimu ambaye ni Prof...., yupo pia mkurugenzi mkuu wa HESLB, na Mkurugenzi wa Fedha wa HESLB. Hao watakuambia A-Z ya program hii kwasababu ni kama miaka 2 sasa toka waliposafiri na timu yao kuja Ujerumani kwa kodi zetu kwa kile walichokiita kuja kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa matatizo yetu hasa namna ya kuweza kuwalipa wanafunzi hawa stipend allowances zao kama mkataba unavyoonyesha. Hatahivyo, hatujaona matunda ya safari yao, kwani mpaka sasa matatizo ndiyo yamezidi. Nasema yamezidi kwani kabla ya kuja kwao angalao waliotutangulia walikuwa wakilipwa japo katika kipindi cha mwezi hivi. Hii ni tofauti na sasa ambapo kuna baadhi yetu hawajalipwa Stipend allowances zao za mwezi Oktoba, Novemba, na Desemba 2015. Pamoja nao, wale wote wenye familia huku ujermani wana miezi 3 (Oktoba-Desemba 2015) bila kulipwa pesa hizo.

AJABU LA MWAKA:
Mh. Rais, katika suala hili kumekuwa na mambo ya ajabu sana hasa kutoka kwa watendaji wa HESLB (Mkurugenzi wa Fedha). Huyu bwana amekuwa akitudanganya sana toka mwezi Oktoba 2015 kuhusu malipo yetu. Imefikia hatua wanaandaa majina yetu pale ofisini kwao na kiasi tunachopaswa kulipwa na kuonyesha kwamba tayari pesa zimepelekwa Benki. Sisi waathirika tunakaa kama wiki nzima bila kuona pesa kwenye akaunti zetu, na kiongozi wetu huku Ujerumani akifuatilia anaambiwa kuna kosa lilitendeka, hivyo, malipo yatanyika muda sio mrefu. HESLB chini ya Mkurugenzi Mtendaji na Mkurugenzi wa Fedha wametudanganya sasa zaidi ya mara 3 sasa kwamba pesa zimeshatumwa wakati ni UONGO. Hii hali imetusababishia usumbufu mkubwa sana katika mambo yetu ya kielimu na hata kijamii. Hata leo kiongozi wetu huku ujerumani alikwenda wizara ya Elimu baada ya kudanganywa tena na HESLB kwamba tungelipwa pesa zetu wiki iliyopita. Huko kote hakuna mafanikio, kwani bado ameambiwa tuandike tena barua japo suala letu linajulikana sana pale wizarani, TCU na HESLB.

Mh., Rais,
Hakika tunaumia sana na kwa hakika hatujui nini cha kufanya sasa, kwani shule na njaa na usumbufu wa kodi za pango ni mkubwa sana kwetu. Charges nazo zimekuwa nyingi sana na mbaya zaidi sasa tumekuwa ombaomba hadi wametuchoka. Kuna hoja hapa labda kuhusu sisi kutafuta kibarua huku ili tuweze kujikimu, hilo kwanza lina implications katika kusoma kwetu lakini pia mkataba wetu unatuzuia kufanya kazi. Kwa program hii ni kwamba Wizara ya Elimu kupitia TCU na HESLB inatakiwa kutulipa 80% ya Stipend allowances zetu na DAAD ya Ujerumani inalipa 20% pekee. Kwa 20% ya DAAD haitoshi hata gharama ya Chumba achilia gharama ya kula na hata registration fees.

Mh. Rais, kwa namna ya kipekee sana tunaomba utusaidie, kwani tuna hali mbaya sana. Hatujapata Stipend allowances ya Miezi 3 (Oktoba-Desemba 2015) pamoja na Family allowances ya miezi hiyo.

Natanguliza shukrani na tunaangalia mbele kwa matumaini ya suala letu kupata ufumbuzi mapema.

Ahsante sana na nikutakie kila la kheri katika ujenzi wa Taifa letu pendwa la Tanzania.

Ndimi, muhathirika wa HESLB/TCU/Wizara ya Elimu.



No comments :

Post a Comment