Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, January 3, 2016

Askofu: Magufuli kafanya tuumalize 2015 kwa raha

Rais John Magufuli    
By Daniel Mjema, Mwananchi
Moshi. Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Afrika Mashariki (KKKAM), Jesse Angowi amesema Rais John Magufuli amewapa raha Watanzania walipokuwa wakiumalizia mwaka 2015 na kumtaka aongeze bidii zaidi mwaka huu.
Askofu Angowi alitoa kauli hiyo juzi katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Uchira, Moshi Vijijini alikohudhuria sherehe za Kipaimara.
Alimtaka Rais Magufuli kuendelea kutumbua majibu sugu yaliyoota katika sekta mbalimbali za Serikali.
“Rais Magufuli na Waziri mkuu wake (Kassim Majaliwa) ni wa kuwapigia makofi kwa kile walichokifanya pale bandarini Dar es Salaam, lakini asiishie hapo, ahamie pia kwenye vituo vingine vya forodha,” alisema.
Alisema Rais Magufuli na watendaji wake wanapaswa pia kuchunguza ufisadi mwingine ambao uko katika uingizaji wa mafuta yanayoshushwa kwenye bandari za Dar es Salaam na Tanga.
“Hili nalo ni jipu lingine kwa sababu kuna visingizio visivyo na tija, mara nyingine huwa tunaambiwa eti mita zilizonunuliwa kwa mabilioni ya shilingi kwa ajili ya kupima mafuta yanaposhushwa hazifanyi kazi, hii ni hujuma. Aende huko nako,” alisisitiza.
Alisema kazi inayofanywa sasa na Serikali ni kutaka kurudisha uchumi wa nchi ambao ulianza kumilikiwa na watu wachache kwa manufaa yao binafsi.
Alisema rasilimali za nchi zinapaswa kumilikiwa na Watanzania wote badala ya kundi dogo la watu.
Mmoja wa waumini wa Kanisa hilo, Elia Kimaro alisema kazi anayoifanya Rais Magufuli na Waziri mkuu ni ngumu kwa sababu inagusa maslahi ya mafisadi waliokuwa wamejilimbikizia mali.
“Hawa watu kwa kweli ikibidi waongezewe ulinzi,” alisema.
Kimaro ambaye pia ni mpigapicha mkuu wa kanisa hilo, alimuomba Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman kuufanyia mabadiliko muhimili wa Mahakama ili watumishi wasio waadilifu wanaoshiriki ufisadi na rushwa waondolewe.     

No comments :

Post a Comment