Jaji Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Othman Makungu(kulia) Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Said Hassan Said (kushoto) na Mshauri wa Rais Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bw.Abrahman Mwinyijumbeni miongoni mwa viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Mshauri wa Rais Utamaduni,Katibu Tume ya Mipango,naibu katibu Wizara ya katiba na Sheria na Katibu Kamisheni ya Utumishi wa Umma leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw. Juma Hassan Reli kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo,kabla alikuwa Naibu Gavana wa Benki ya Tanzania.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw. Mdungi Makame Mdungi kuwa Katibu Kamisheni ya Utumishi wa Umma katika hafya iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw. Kai Bashir Mbarouk kuwa Naibu Katibu Wizara ya Katiba na Sheiria katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini pia walihudhuria katika hafla ya kuapishwa Mshauri wa Rais Utamaduni,Katibu Tume ya Mipango,naibu katibu Wizara ya katiba na Sheria na Katibu Kamisheni ya Utumishi wa Umma leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Said Hassan Said (kushoto) na Mshauri wa Rais Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bw.Abrahman Mwinyijumbeni miongoni mwa viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Mshauri wa Rais Utamaduni,Katibu Tume ya Mipango,naibu katibu Wizara ya katiba na Sheria na Katibu Kamisheni ya Utumishi wa Umma leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw. Chimbeni Kheir Chimbeni kuwa Mshauri wa Rais Masuala ya Utamaduni hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
Baadhi ya Makatibu katika taasisi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar waliohudhuria katika hafla ya Kiapo kwa wateuliwa na Rais wa Zanzibar walioapishwa leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja (Picha na Ikulu)
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 15 Januari, 2016
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amemwapisha Bwana Chimbeni Heri Chimbeni kuwa Mshauri wa Rais Masuala ya Utamaduni kufuatia uteuzi alioufanya hapo jana ambapo aliteua pia watendaji wengine wa serikali.
Watendaji wengine walioapishwa leo ni Bwana Juma Hassan Juma Reli kuwa Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango, Bwana Mdungi Makame Mdungi kuwa Katibu Kamisheni ya Utumishi wa Umma na Bwana Kai Bashir Mbarouk kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria.
Bwana Reli ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo ya Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania anachukua nafasi ya Bi Amina Khamis Shaaban ambaye hivi karibuni aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Kabla ya uteuzi wa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma bwana Mdungi alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba Sheria.
Kwa upande wa Bwana Kai Bashir kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Wizara hiyo.
Hafla hiyo fupi iliyofanyika Ikulu ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Said Hassan Said.
Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dk. Mwinyihaji Makame, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Mheshimiwa Haroun Ali Suleiman, Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Maalim Abdulla Mwinyi na Makatibu na Manaibu Katibu wakuu wa wizara mbalimbali.
Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822
No comments :
Post a Comment