Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, January 5, 2016

Hali ya Hewa: Joto Dar si la kawaida

Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi.
By Florence Majani, Mwananchi
Dar es Salaam. Joto kali lililoikumba mikoa ya pembezoni mwa Bahari ya Hindi hasa Dar es Salaam imeelezwa kuwa si la kawaida kutokana kiwango cha wastani cha joto duniani.
Imeelezwa kuwa hali hiyo imesababishwa na ongezeko la joto katika eneo la Bahari ya Pacific, ambako mzunguko wa hali hewa umesogea zaidi katika eneo la Pwani ya Bahari ya Hindi.
Desemba mwaka jana, joto lilikuwa kubwa kuliko miezi mingine na lilipanda kwa asilimia 2.5 ya kiwango cha wastani cha nyuzi joto 32.
Meneja wa Huduma za Utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Samwel Mbuya alisema joto limeongezeka kuliko kipindi kilichopita yaani mwaka 2013 na 2014, ingawa hata kwa miaka hiyo kiwango hicho kilivuka wastani wa kawaida.
“Kipindi hiki cha Desemba, Januari na Februari, joto huongezeka, lakini kuwapo kwa El-Nino na ongezeko la joto la bahari kutoka Bahari ya Pacific, kumechangia ongezeko la joto Bahari ya Hindi,” alisema.
Wakati huohuo, Shirika la Hali ya Hewa Duniani, limetangaza kuwa mwaka jana ulikuwa na joto lililozidi kiwango wastani joto cha duniani.
Mamlaka hiyo ilieleza kuwa hilo ni joto ambalo lipo juu kulinganisha na lile la 2014, ingawa hata la mwaka huo nalo halikuwa la kawaida.
Mbuya alisema ongezeko hilo la joto halijaleta mvua kama inavyotakiwa, badala yake limeleta joto la fukuto. Hali hiyo imesababisha hata viwango vya joto ambavyo si vikubwa kuleta madhara makubwa.
Septemba mwaka jana, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi alitoa tahadhari ya kuwapo kwa mvua za El-Nino kutokana na mabadiliko ya joto katika Bahari ya Pacific na kubaini kuongezeka kwa joto ambalo sasa limefikia nyuzi joto 2.5 juu ya wastani.
Hata hivyo, Mbuya alisema TMA haijafanya ulinganifu wa kiwango cha joto katika miji mingine ya Afrika na jiji la Dar es Salaam.
“Bado tunafanya ulinganifu na baada ya mvua za vuli, tutaangalia nini kitaonekana kwenye rekodi kwa maana ya ikiwa viwango hivyo vimepita vya miaka ya nyuma,” alisema.
Mei mwaka jana, watu zaidi ya 500 walifariki dunia katika jiji la Allahabad, India baada ya joto kufikia kiwango cha nyuzi 50.

No comments :

Post a Comment