Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam mara baada ya kukutana kwa mazungumzo mafupi na Rais Dk. John Magufuli, Ikulu na baadhi ya mawaziri, alisema wamekubaliana kuimarisha uhusiano na maeneo muhimu ya kuwekeza.
Alisema ofisi hiyo ndogo itafunguliwa hivi karibuni na itashughulikia masuala ya visa kwa kuchukua taarifa muhimu za waombaji, kuzituma ubalozini jijini Nairobi Kenya, na kwamba itachukua siku saba hadi 10 kwa muhusika kupata visa.
Aliyataja maeneo waliyojadiliana na rais na mawaziri kuwa ni ulinzi na usalama, kilimo, mawasiliano, nishati na biashara, na kwamba Septemba mwaka huu, ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Tanzania watatembelea nchi hiyo kuangalia fursa zilizopo.Vilan alisema katika kuhakikisha uhusiano baina ya nchi hizo hauyumbi, kila mwaka ujumbe wa wafanyabiashara, watalaam na wadau wa sekta mbalimbali hutembelea nchi hiyo na wengine kuja nchini.
“Israel haina ubalozi hapa nchini kutokana na sababu za kiuchumi kushindwa kuhudumia, kama inavyofahamika kwa Afrika kulikuwa na Balozi zaidi ya 30 ila kwa sasa zimebaki tisa…lakini tunaimarisha mahusiano na Tanzania kwa kutembeleana na kushirikiana kwa mambo muhimu ya nchi zetu,” alisema.
Balozi huyo ambaye yupo nchini kwa ziara ya siku tatu, alisema katika sekta ya kilimo wameshirikiana kwa Watanzania kwenda kujifunza masuala mbalimbali ya kilimo cha asali, na kwamba kwa sasa watapeleka Watanzania wengi kujifunza katika masuala la kuwezesha wanawake, kilimo, elimu na biashara.
Aidha, alimshukuru Rais Magufuli kwa mapokezi na kuonyesha nia ya kushirikiana kwa karibu zaidi na nchi hiyo katika sekta mbalimbali na kuhakikisha nchi husika zinanufaika kwa maendeleo endelevu ya watu wake.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment