Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, January 20, 2016

Jengo la ghorofa nne Dar latishia maisha

Siri kubwa imejificha kuhusu ujenzi wa jengo la biashara na makazi unaoendelea mtaa wa Mchikichi, Kariakoo jijini Dar es Salaam ambalo limesababisha sehemu ya ghorofa lililopo mkabala nalo kutitia.

Wakati mkandarasi wa jengo linalojengwa, Salum Nassor, akisema taratibu zote za ujenzi zimefuatwa, mmiliki wa eneo, P.M. Aloyce, amewahamisha wapangaji na wamiliki wa ghorofa hilo juzi kutokana na hofu ya kudondoka.
 
Akizungumza na Nipashe nje ya jengo hilo, mkandarasi Nassor alikiri sehemu ya nyumba yenye ghorofa nne lililopo mkabala na eneo analolisimia kwa ujenzi, kupata tatizo.
 
Alisema nyumba hiyo ambayo imepata tatizo hilo ni ya muda mrefu na kwamba Jumamosi walipoanza kuchimba siku iliyofuata, waliona sehemu ya baraza la nyumba hiyo ikititia.
 
“Tumeanza kuchukua hatua kwa kuvunja baraza ili lisisababishe madhara, tutalijenga upya, kitaalam nyumba na nyumba zinatakiwa ziache mita tatu, ila ujenzi wa huku si mnaujua, pale wanashirikiana alama za mipaka,” alisema.Aidha, alisema mmiliki wa ujenzi anaousimamia, alikutana na wapangaji pamoja na wamiliki nyumba hiyo ya ghorofa na kuwataka wahame na atawalipia kodi wanakokwenda kupanga.
 
“Alifanya hivyo baada ya hofu kutanda kuwa ghorofa litaanguka, jana (juzi), kilichotokea ni kwamba baada ya watu hawa kuhama, nimesikia ahadi haikutimizwa ya kuwalipia nyumba walizopata, ndiyo maana simu zikapigwa kwenu, yeye alimwaga mboga wao wamemwaga ugali,” alisema.
 
Alibainisha kuwa nyumba hiyo haitadondoka kwa sababu kitaalam tendo hilo lisingechukua zaidi ya saa 12.
 
Alisema ujenzi unaoendelea hivi sasa ni kukarabati baraza iliyotitia, kisha waendelee na ujenzi.
 
“Ujenzi wa hapa umeanzia chini tofauti na nyumba hii ya zamani ambayo ulikuwa wa kawaida,” alisema.
 
Msimamizi Mkuu wa ujenzi huo, Maneno Mbeyu, alisema jengo ambalo baraza lake limetitia, ujenzi wake ulishuka chini mita tatu wakati wakwao ni mita nne.
 
Alisema baada ya kufika mita nne, ndiyo sehemu ya baraza ya ghorofa hilo iliyokuwa na familia zaidi ya 15 ikaanza kutitia.
 
Mkuu wa Operesheni kutoka Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji, Emmanuel Kibona, alisema hatua za awali walizochukua ni pamoja na kuvitaka vibali vya ujenzi wa majengo hayo ili wavichunguze.
 
Mmoja wa wamiliki wa sehemu ya jengo hilo lililotitia, Mohamed Zakaria, alisema walianza kuona ufa ulioanzia mbele ya jengo hilo kuelekea nyuma.
 
Alisema baada ya kuona hivyo, waliwahamisha watu waliokuwa juu ya jengo hilo kwa madai ya kuwalipia pango.
 
Mjumbe wa shina namba 7, Kariakoo Mashariki, Ramadhan Nassor, alisema anachojua ni kwamba baada ya tatizo hilo, mmiliki wa ujenzi unaoendelea aliwataka watu wahame kwa gharama zake.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment