dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, January 17, 2016

Kuzuia mikutano ya walioshindwa Waziri Mkuu kapotoka

 Image result for kassim majaliwa
By Peter Saramba
Tangu ateuliwe, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amejitwalia sifa na umaarufu kutokana na jinsi anavyokwenda kwa kasi ya “Hapa Kazi Tu” ya mteuzi wake, Rais John Magufuli.
Kama alivyo Rais Magufuli, Waziri Mkuu Majaliwa naye ameingia madarakani kwa staili ya ziara za kushtukiza zinazoambatana na hatua za papo hapo dhidi ya watendaji wanaobainika kutotimiza wajibu.
Hata hivyo, usemi wa wahenga kuwa mgema akisifiwa tembo hilitia maji inaanza kuonekana katika kauli ya Waziri Mkuu wetu baada ya kukaririwa akidai wagombea walioshindwa kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita hawastahili kuitisha na kuhutubia mikutano ya hadhara kuwashukuru wananchi.
Binafsi pamoja na kumkubali Waziri Mkuu Majaliwa kwa kasi yake ya kiutendaji alioanza nayo, lakini katika hili sikubaliani naye, simuungi mkono na ninaamini amepotoka.
Aidha, kapotoka kwa ushauri mbaya kutoka kwa washauri na wasaidizi wake, au kapotoka yeye mwenyewe kwa kuelemewa na sifa.
Kama ambavyo anakiri kuwa waliogombea na kushinda wanastahili kuitisha mikutano ya kuwashuruku wananchi kwa kuwachagua, Waziri Mkuu anapaswa kutambua kuwa hata walioshindwa (siku hizi wanasema kura hazikutosha), pia wana haki hiyo.
Ibara ya 20 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inatoa haki ya kujumuika kwa raia nchi hii bila kujali makundi yao ya kijamii ili mradi jumuiko hilo halikiuki sheria.
Hata sheria ya vyama vya siasa inayoruhusu mfumo wa vyama vingi vya siasa pia inatoa fursa kwa vyama vyote vyenye usajili kuendesha shughuli za kisiasa ikiwamo kuitisha na kuhutubia mikutano ya hadhara kunadi sera kutafuta uungwaji mkono na wananchi.
Kwa misingi hiyo, uhuru wa kujumuika ni wa kikatiba na kisheria. Hauwezi kuzuiwa siyo tu na Waziri Mkuu, bali na mtu awaye yote au chombo chochote nje ya utaratibu wa kisheria.
Kuzuia uhuru huo ni kuvunja katiba, na hilo ni kosa kubwa. Ukubwa wa kosa hilo unaongezeka pale mtendaji anapokuwa mtu aliyeapa kuilinda, kuitetea na kuhifadhi Katiba kama Waziri Mkuu Majaliwa.
Ni kweli wapo walioshinda na walioshindwa Uchaguzi Mkuu uliopita. Hata hivyo, kushinda hakuongezi haki ya kisiasa kwa washindi dhidi ya washindwa.
Washindi na washindwa wote wanaendelea kuwa na haki sawa ya kujumuika na wapiga kura wao, kuwahutubia kwenye mikutano ya hadhara kuwashukuru kwa kidogo walichopata.
Kwa mfano, Rais Magufuli ameshinda nafasi hiyo kwa kura zaidi ya 8 milioni dhidi ya msindani wake wa karibu Edward Lowassa aliyejikusanyia kura zaidi ya 6 milioni.
Ushindani miongoni mwa wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani pia ulikuwa vivyo hivyo katika majimbo na kata kadhaa nchini.
Kusema Rais Magufuli ana haki ya kukutana na wananchi kwenye mikutano ya hadhara na kuwashukuru kwa kura zaidi ya 8 milioni walizompigia, lakini Lowassa na wagombea wengine walioshindwa wakose haki hiyo ni kupotoka kikatiba na kisheria.
Mtu mwenye wadhifa wa Uwaziri Mkuu siyo wa kupotoka kwa kiwango hicho.
Ingawa ni kweli Serikali ina haki na wajibu wa kuwatumikia wananchi baada ya uchaguzi kukamilika. Haki na wajibu huo hauondoi haki ya kikatiba ya makundi mengine.
Ni haki na wajibu! Lakini haki na wajibu huo wa serikali haondoi haki ya makundi mengine ya kisiasa, wagombea na vyama shindani vya siasa vikiwamo.
Kwa misingi na haki ile ile ya washindi kushukuru ndivyo washindwa nao wanapaswa kupewa fursa hiyo bila kuwekewa vikwazo nje ya utaratibu wa kikatiba na kisheria.
Kama ambavyo Rais Magufuli ana haki kuwashukuru wapiga kura wake zaidi ya 8 milioni, ndivyo hivyo Lowassa naye anastahili kuwashukuru Watanzania zaidi ya 6 milioni waliomwamini na kumpigia kura zao.
Wingi au uchache wa kura kisiwe kigezo cha kuruhusu au kupiga marufuku mikutano ya kisiasa nchini. Kufanya hivyo ni kuvunja Katiba na sheria.
Ingawa bado siamini, lakini kauli ya Waziri Mkuu Majaliwa inaibua sintofahamu kuhusu tuhuma za wanaosadikiwa kuwa wana CCM jimboni mwake kung’oa bendera za vyama vingine shindani jimboni humo.
Ingawa ni kweli mshindi katika Jimbo la Ruangwa ni Kasima Mmajaliwa, lakini hiyo haiondoi haki ya wagombea na vyama vingine kufanya shughuli za kisiasa jimboni humo.
Sina ushahidi wa kimahakama kama Waziri Mkuu yuko nyuma au anaunga mkono wafuasi wake kung’oa bendara za vyama vingine jimboni kwake, lakini kauli yake ya kuzuia mikutano ya hadhara ya wagombea na vyama vilivyoshindwa inabeba ujumbe mzito.
Washauri na wasaidizi wake wamsaidie kuepuka upotokaji wa aina hii kwa sababu inafifisha sifa, haiba na imani yake kwa umma unaonza kumwamini kiutendaji. Mungu ibariki Tanzania!
0766 434 354.     

No comments :

Post a Comment