dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, January 17, 2016

TCRA kufungia vituo sita vya televisheni, redio 20

Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy
By Kalunde Jamal, Mwananchi
Dar es Salaam. Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), imevifungia kwa miezi mitatu, vituo sita vya televisheni na vingine zaidi ya 20 vya redio hadi pale vitakapolipa ada mbalimbali.
Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy alivitaja vituo hivyo kuwa ni Star TV, Sumbawanga TV, Tanga TV, Mbeya TV na Mussa Television Network.
Redio Uhuru, Kiss FM, Redio Free Africa, Breeze FM, Counntry FM, Generation FM, Hot FM, Redio Sengerema, Impact FM, Iringa TV, Rock FM, Kifimbo FM, Sibuka FM, Kili FM, Pop FM, Ulanga FM, Kitulo FM, Standard FM, Pride FM na Huruma Redio.
Alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya kuwatumia taarifa ya kulipa madeni wanayodaiwa ndani ya mwezi mmoja, Julai 21, mwaka jana, lakini hadi Septemba 28 walikuwa hawajalipa na kutumiwa taarifa nyingine ya kuwataka kufanya hivyo.
Hata hivyo, Meneja wa Redio Uhuru, Angela Akilimali alisema hawajafungiwa kama inavyoelezwa, bali wamepewa taarifa ya kulipa deni ndani ya miezi mitatu, iwapo hawatalipa deni watakatiwa matangazo.
“Madeni hayo siyo mapya ni ya zamani hata kabla sijakaa katika nafasi hii nimeyakuta, tutalipa ndani ya miezi hiyo mitatu waliyosema,” alisema.
Mmiliki wa Sahara Media Group, inayomiliki vituo vya Star Tv, Redio Free Afrika, Anthony Diallo alisema hawajapata taarifa za kudaiwa na mara ya mwisho alipokutana na TCRA aliwalalamikia kuwapa ankara ya malipo kwa dola badala ya shilingi.
“Hatujapata taarifa rasmi, kama wameita waandishi wa habari wakazungumza nao bila kuwaambia wahusika ambao ni sisi. Wanatuchafulia jina ilhali matatizo ya msingi hawajamaliza,” alisema Diallo.
Akizungumzia madai hayo, Mungi alisema walitumiwa taarifa ya mara ya pili pamoja na kuwakumbusha kulipa kwa kuwatumia gharama wanazodaiwa huku wakiongezewa muda kabla ya Desemba 31, lakini hakuna aliyelipa.
Alisema kila kampuni katika hizo zilizotajwa imepelekewa taarifa na wahusika wamesaini kuzipata.
Kuhusu kupelekewa ankara kwa dola, Mungi alisema sheria ya ankara za malipo ipo hivyo lakini kulipa ni kwa shilingi na kwamba hakuna ambaye aliwahi kukataliwa kulipa kwa sababu hana fedha za kigeni.
Alisema wataendelea kurusha matangazo lakini; “ikifika saa sita kamili usiku wa kuamkia kesho, vituo vyote nilivyovitaja tutakuwa tumevifungia matangazo, ingawa atakayelipa kabla ya muda huo ataendelea kubaki hewani,” alisema Mungi.     

No comments :

Post a Comment