Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, January 3, 2016

Mabwepande wamvulia kofia Magufuli


Baadhi ya wakazi wa Mabwepande jijini Dar es Salaam, wamefagilia kasi ya Rais John Pombe Magufuli wakisema kuwa mwendo anaokwenda nao umewanyoosha watendaji waliokuwa wanafanyakazi kwa mazoea.

Wakizungumza na Nipashe juzi, wananchi hao walisema Rais Magufuli amepatikana kwa mpango wa Mungu ndiyo maana kwa kipindi kifupi alichokaa madarakani amefanya mambo makubwa ikiwa ni pamoja na kuokoa fedha nyingi zilizokuwa zikiliwa na wachache.

Bisikina Mitandi anayeishi mji mpya, Mabwepande, alisema utendaji wa Magufuli unapaswa kuigwa na watendaji wake popote watakapoona udhaifu ndani ya uongozi wao wawawajibishe mara moja watumishi wazembe.

“Rais ameokoa mamilioni ya fedha yaliyokuwa yakipotea kila siku kutokana na usimamizi mbovu, tumeshuhudia wafanyabiashara wakubwa ambao walikuwa wamekwepa kodi lakini wamelipa wenyewe,” alisema.

Mitandi alisema jambo lingine linalofanya wananchi wamfurahie Rais Magufuli ni hatua yake ya kuagiza  fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe mbalimbali za kiserikali zielekezwe kwenye matumizi mengine ya huduma za kijamii kama kununua vitanda na kujenga barabara.

Mjumbe wa mtaa wa Mlimani City, Mabwepande, Rashid Nampanda, aliwataka watendaji ndani ya serikali kufuata nyayo zake kwa kufichua wabadhirifu wa fedha za umma.

“Kuanzia ngazi zetu za ujumbe wa serikali za mitaa tunatakiwa kumuunga mkono Rais ili nchi isonge mbele maana ameonyesha njia na anatujali wananchi wake,” alisema.

Naye, Salima Said alisema kasi ya utendaji wa Rais Magufuli ikiigwa na watendaji wake kwa uadilifu, ipo siku Tanzania itaacha kuwa ombaomba kwa nchi wahisani.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment