Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, January 2, 2016

Majaliwa aahidi kutimiza ahadi 100%

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Waziri MKUU Kassim Majaliwa (pichani) amewataka Watanzania kuendelea kumuunga mkono Rais John Magufuli katika kutumbua majipu na kuahidi kwamba ahadi zote alizotoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana zitatekelezwa.
 
Waziri Mkuu alitaka Watanzania kuendelea kuwa na imani na Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwa itatimiza ahadi zote ambazo Rais na Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu walizitoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.
Aliyasema hayo jana Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu wapya.
 
Aidha, Majaliwa aliwapongeza Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu ambao jana waliapa na kutia saini ‘hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma’ mbele ya waandishi wa habari. Waziri Mkuu pia alitaka viongozi hao kuwa waaminifu, kuwajibika na kutoa taarifa ya utendaji kwa wananchi.Aidha, Waziri Mkuu alisema viongozi wengine watakao apa kiapo hicho mbele ya Kamishna wa Tume ya Maadili ni pamoja na Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri, ikiwa ni hatua ya Serikali kudhibiti na kufuatilia matumizi ya rasilimali fedha.
 
“Wakuu wa Wilaya watahakikisha fedha zilizoenda katika Halmashauri zao lazima zitumike katika shughuli zilizokusudiwa,” alisema Majaliwa.
Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu hao, waliapishwa na Rais Magufuli, ambapo shughuli hiyo ilihudhuriwa pia na Makamu wa Rais, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Mke wa Mheshimiwa Rais mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi mbalimbali.
 
Kuapishwa kwa Makatibu na Manaibu Makatibu ni kukamisha uundaji wa serikali baada ya Rais kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Mawaziri kwa awamu mbili Ikulu mwishoni mwa mwaka jana.
 
Baraza la Mawaziri la Rais Magufuli lina Wizara 18 na Mawaziri 19, wakati Makatibu Wakuu ni 29.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment