dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, January 24, 2016

Marubani waombewa m10/- wasome

Image result for TANZANIA Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT)

Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT), kimesema gharama ya kumsomesha mwanafunzi wa urubani na wahandisi wa ndege ni Sh.milioni 10 hivyo kimeiomba serikali kupitia Bodi ya Mikopo iweze kuwasaidia wanafunzi wanaochukua kozi hizo. 

Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji Mhandisi Dk. Zacharia Mganilwa, wakati wa uzinduzi wa 'Banda' la ndege litakalotumika katika mafunzo ya wahandisi wa ndege na marubani.

Alisema gharama hizo ni kubwa kulinganisha na kozi nyingine zinazotolewa hapa nchini.

Alisema Bodi ya Mikopo imekuwa ikitoa mkopo usiozidi Sh. milioni 1.5 kwa mwanafunzi ambaye ada yake ni Sh. milioni kumi.

Mganilwa alisema gharama kubwa zimekuwa zikibebwa na mzazi, zaidi ya Sh. milioni tisa.

“Sh. milioni tisa ambazo anatakiwa alipe mzazi imekuwa kwa kiasi fulani changamoto kwao hivyo ninaomba bodi ya mikopo iweze kuliangalia suala hili, waongezewa hata kidogo,” alisema.

Mganilwa aliongezea kuwa kwa hivi sasa marubani wengi na wahandisi wa ndege wamezeeka na wengine kustaafu hivyo kuiacha sekta ya anga kuwa na Watanzania wachache na wengi wageni.

“Mipango na mikakati yetu mikubwa ni kuona tunazalisha watanzania wengi kabisa katika eneo hili la mafundi wa ndege na marubani, hatutaki kuachia wageni tu waweze kuajiliwa katika sekta hii ya anga nchini,” alisema.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzola, alisema serikali itatoa kila aina ya msaada kwa NIT ili kiweze kuzalisha marubani na wahandisi wa ndege wa kutosha katika kukuza sekta ya anga nchini.

Profesa Kamuzola alisema serikali itashirikiana na Sekta binafsi katika kukisaidia chuo hicho kiweze kufikia malengo yake ya uzalishaji wa rasilimali watu katika sekta ya usafirishaji.

“Tumesikia kutoka kwa mkuu wa chuo hiki kuwa ada ya kumfundisha rubani wa ndege ama mhandisi ni Sh. milioni kumi, lakini tukimpeleka mwanafunzi nje ya nchi tutapaswa kulipa ada ya zaidi ya Sh. milioni 100, sasa serikali imewasikia,” alisema.

Aliongeza kuwa kwa kutoa mafunzo haya kwa gharama ya bei nafuu kabisa, ana imani kwamba Watanzania wengi wenye nia ya kusomea urubani na uhandisi wa ndege watajiunga na chuo hicho.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment