dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, January 17, 2016

Mawakala wataka tume wizi kontena 11,000

Image result for bandarini


Sakata la makontena zaidi ya 11, 000 yaliyotolewa Bandari Kavu (ICD’s) bila kulipiwa tozo ya Mamlaka ya Bandari (TPA), limechukua sura mpya baada ya Chama cha Mawakala wa Forodha (Taffa), kuwasilisha kwa Waziri ushahidi wa malipo waliyofanya kwa Bandari.

Aidha, Taffa inataka kuundwa kwa tume huru ya uchunguzi ili kupata ukweli wa sakata hilo.

Wanachama wa Taffa walituhumiwa na TPA kwamba walipitisha makontena hayo bila kulipia tozo ya bandari, lakini wenyewe wamekuwa wakikanusha na kuwarushia lawama watumishi wa bandari na benki ya CRDB.

Akizungumza na Nipashe jana, Katibu Mkuu wa (Taffa), Tony Swai alisema unahitajika umakini wa hali ya juu wakati wa kulishughulikia jambo hilo ili ukweli uweze kufahamika na wahusika kuchukuliwa hatua kali.

Alisema wanachama wa chama hicho wameshawasilisha vielelezo vyao vyote kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kwa ajili ya kumsaidia kubaini ukweli.

“Wanachama wetu walilipia tozo na nyaraka zote wanazo na wamepeleka kwa Waziri kama ushahidi, tumeomba iundwe tume maana ndiyo itabaini pumba ziko wapi na mchele uko wapi," alisema Swai.

"Hatuwezi kusema kwamba wanachama wetu wote wako safi maana waswahili wanasema msafara wa mamba kenge nao wamo, lakini kwa hili ushahidi wa malipo yote tuliyofanya upo thabiti.”

Alisisitiza kuwa tume hiyo ndiyo itakuwa na uwezo wa kubaini watu waliokula fedha zilizotokana kwa malipo  ya tozo hiyo, na kwamba utaratibu wa sasa wa kila taasisi kufanya uchunguzi wake hautakuwa na manufaa yoyote.

Alisema ni vyema na ikaundwa tume itakayoishirikisha wajumbe kutoka Taffa, Taasisi ya Usalama wa Taifa(TISS), Mamlaka ya Bandari (TPA), Benki ya CRDB na  Polisi ili kuchunguza nani hasa walihusika na utolewaji wa kontena hizo bila kulipiwa tozo za bandari na kusababisha upotevu wa mamilioni ya fedha za umma.

Katibu huyo alisema katika hali ya kawaida, wakala wa forodha hawezi kutoa kontena kwenye bandari kavu bila mmiliki wa bandari hiyo kuthibitisha malipo yaliyofanywa kwenye benki ya CRDB.

“Mwenye ICD akishajiridhisha kwamba umelipa tozo ya TPA ndipo nayeye anakupa gharama za kuhifadhi mzigo wako kwenye bandari yake kisha unachukua mzigo wako," alisema Swai.

"Sasa cha kujiuliza waliruhusu vipi kontena (11,000) zitoke bila kulipiwa tozo za TPA? Nani wanahusika na walifanyaje fanyaje?
"Tume huru pekee ndiyo itakuja na majibu ya mchezo wote huu.”
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment