Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, January 25, 2016

Mbunge wa CCM amvaa Membe

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ( Kushoto), Mbunge wa Nzenga Mjini (CCM), Hussein Bashe (Kulia)
By Kelvin Matandiko, mwananchi
Dar es Salaam. Mbunge wa Nzenga Mjini (CCM), Hussein Bashe amemtaka aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kuacha kumshambulia Rais John Magufuli katika utendaji wake.
Kauli ya Bashe imekuja siku moja baada ya mfululizo wa habari zilizomnukuu Membe akimkosoa Rais Magufuli katika maeneo kadhaa likiwamo suala la kuzuia safari za nje, Rais kwenda nje ya nchi huku akimpa tahadhari ya kuwashughulikia wafanyabiashara wakubwa.
Kupitia taarifa yake kwenye mitandao ya kijamii, Bashe alisema Membe amekuwa waziri kwa miaka kumi na kutimiza wajibu wake, hivyo amuache Magufuli naye atimize wajibu wake kwa wananchi.
“Aliomba urais, hajateuliwa, asubiri 2020 au 2025 ili akipita aanzishe ‘uvasko da Gama’ tena,” alisema.
Alisema hoja alizotoa kumkosoa Rais Magufuli zinaonyesha ni mwanasiasa mufilisi. “Serikali haijapungua, kubwa au ndogo au hoja kuwa safari za nje ni muhimu na Rais amekosea kufuta ama kupunguza ni hoja ya mwanasiasa muflisi.”
Bashe alisema mwansiasa huyo akisema amefaidika na safari za nje yeye binafsi bila manufaa kwa nchi na amekuwa sehemu ya mfumo dhaifu ulioifikisha Tanzania ilipo kama Taifa, hivyo anatakiwa kutulia kwa kuwa kila Rais ana mtazamo wake.
Alisema Rais Magufuli anaamini matatizo ya Taifa yatamalizwa na Watanzania wenyewe kwa kudhibiti matumizi ya hovyo na yasiyokuwa ya lazima badala ya kutegemea safari za Ulaya zinazoendeleza tabia ya taifa kubakia ombaomba.
Alisema ni muhimu Membe akafahamu kuwa Rais Magufuli ana staili yake na atapimwa kwa kuangalia matokeo, lakini kwa sasa hatujaona athari za zake.
Bashe pia alisema anatambua maamuzi mengi ya Rais Magufuli kwa sasa hayatafurahisha wengi waliofaidika na miradi kama Nida, fedha za Gadafi, na matumizi mabaya ya madaraka katika awamu ya nne.
Alisema majipu mengi yanayosubiri kutumbuliwa ama yaliyotumbuliwa yatafanya jitihada kukosoa mwelekeo wa Serikali ya awamu ya Tano.
Alihoji kwamba hoja ya kutokuwa na mabalozi, haina mashiko kwani Rais Magufuli hajafikisha hata siku 100 ofisini, lakini yeye amekuwa waziri wa Mambo ya Nje kwa miaka minane na hakuona umuhimu wakati huo.
“Binafsi kama mbunge, naunga mkono ‘style’ ya Rais Magufuli ya uongozi, mabadiliko anayofanya sasa yanahitaji roho ngumu, uwendawazimu kidogo, kuungwa mkono na wananchi wote kwa kuwa waliofaidika na udhaifu wa awali watajitahidi kutaka kuzuia mabadiliko,” alisema Bashe.     

No comments :

Post a Comment