dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, January 21, 2016

Serikali yakanusha uzushi Magufuli kufukuza wageni.

Rais Dk. John Magufuli.
Serikali imekanusha uzushi unaosambazwa katika mitandao ya kijamii ya ndani ya nchi na nje ya nchi kuwa Rais Dk. John Magufuli, amewafukuza wageni kutoka nje waliokuwa wanafanyabiashara zao nchini kwa kuwa serikali yake haitaki wageni kufanya biashara nchini.
 
Taarifa iliyotolewa na Ikulu jijini Dar es Salaam kwa vyombo vya habari jana ilisema serikali haijafukuza wageni kutoka nje ya nchi kufanya biashara nchini na haina mpango wa kuwafukuza wageni wanaoishi nchini kwa vibali vilivyotolewa kisheria na Idara ya Uhamiaji.
 
"Uzushi huo usiokuwa na ukweli umeenezwa kufuatia Idara ya Uhamiaji kutekeleza jukumu lake la kufuatilia wageni wote wanaoishi nchini bila vibali halali vya ukaazi ambapo kwa mwezi Novemba na Desemba, mwaka 2015 wageni 372 walioondoshwa nchini," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.Ilifafanua kuwa kazi ya kufuatilia wageni wanaoishi nchini bila vibali halali vya kisheria, haijaanza katika Serikali ya Awamu ya Tano. 
 
Ilieleza kuwa Idara ya Uhamiaji nchini tangu Januari hadi Desemba, mwaka jana, iliondosha nchini jumla ya wageni 1,642 waliokuwa wanaishi na kufanya shughuli zao nchini kinyume na sheria.
 
"Uzushi unaoenezwa hauna ukweli wowote na hauna nia njema na nchi yetu kwani kati ya mwaka 2014 na 2016, Idara ya Uhamiaji imetoa vibali vya ukaazi (Residence Permits) 40,765 kwa wageni wawekezaji na wafanyabiashara, wageni wanaofanya kazi za kuajiriwa, wageni wanaokuja kwa ajili ya masomo, matibabu, dini, utafiti na wastaafu kuishi na kufanya shughuli zao nchini," iliongeza taarifa hiyo.
 
Ilisema serikali inawakaribisha wageni kuja nchini kuwekeza na kufanya shughuli zao kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi.
 
Ilisema aidha, kuna uzushi unaenezwa kuwa Rais Dk. Magufuli, amepiga marufuku wanawake kuvaa nguo fupi kama njia ya kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi.
 
"Rais tangu aingie madarakani, hajawahi kuagiza wala kutoa tamko kuhusiana na uzushi wa kukataza uvaaji wa nguo fupi ili kupunguza maambukizi ya Ukimwi kama inavyoenezwa katika mitandao ya ndani na nje ya nchi ambayo inanukuu habari hiyo kuwa imeandikwa na Gazeti la Kenya la `The Standard,' ilisema.  
 
Ilisema serikali inautangazia umma kuwa uzushi huo unaomhusu Rais Magufuli umetungwa na watu wasioitakia mema Tanzania kwa lengo la kumdhalilisha Rais na hauna ukweli hivyo watu wasishiriki kuueneza kwa njia yeyote ile.
 
Aidha, taarifa iliekeza kuwa serikali kupitia balozi zake za Kenya na Afrika Kusini, zinafuatilia chanzo cha uzushi huo kuhusu Rais Magufuli kwa kushirikiana na nchi husika na watakaobainika kutunga na kuueneza, watachukuliwa hatua za kisheria.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment