ZEC ilianza kukutana juzi chini Mwenyekiti wake Jecha Salim Jecha na kujadili ajenda moja ya marudio ya Uchaguzi Mkuu.
Taarifa za uhakiza ambazo Nipashe inazo zinasema kuwa ajenda hiyo baada ya kujadiliwa kwa kina na kuibua mjadala mkali, wajumbe sita walipitisha uamuzi huo huku mjumbe mmoja (jina tunalo) akitoka nje ya kikao.
Ilidaiwa kuwa mjumbe huyo alilazimika kuchukua uamuzi huo akikataa kuwa sehemu ya waliopitisha kurudiwa kwa uchaguzi huo.
Kwa mujibu wa Kamishna mmoja ndani ya ZEC ambaye hakutaka kutajwa jina lake liandikwe gazetini kwa kuwa si msemaji, baadhi ya wajumbe walitaka kufahamu kwanza sababu za Mwenyekiti kufuta matokeo bila idhini ya pamoja.
Ilidaiwa kuwa baadhi ya wajumbe waliona kabla mwenyekiti kufuta uchaguzi huo, walitakiwa kukaa kama tume ili kujadili matatizo yaliojitokeza jambo ambalo alidai halikufanyika na kukosekana maamuzi ya pamoja ya ZEC.
Ilidaiwa kuwa baadhi ya wajumbe waliona kabla mwenyekiti kufuta uchaguzi huo, walitakiwa kukaa kama tume ili kujadili matatizo yaliojitokeza jambo ambalo alidai halikufanyika na kukosekana maamuzi ya pamoja ya ZEC.
Aidha, kamishna huyo alisema waraka wa kurudiwa uchaguzi uliwasilishwa na sekreterieti chini ya mwenyekiti wake ambaye ni mkurugenzi wa ZEC na kupendekeza marudio yafanyike Machi mwaka huu.
Tarehe kamili ya uchaguzi itapangwa na kamati tendaji ya ZEC, alisema, baada ya kukamilisha bajeti.
Mwenyekiti ZEC Jecha jana hakuweza kupatikana kuelezea maendeleo ya kikao hicho baada ya simu yake kutopokelewa tangu juzi.
Wakati ZEC ikiamua kurudiwa kwa uchaguzi, kamati ya mazungumzo ilikutana juzi Ikulu mjini Unguja chini ya Mwenyekiti Rais Ali Mohamed Shein lakini hakuna taarifa yoyote iliyotolewa juu ya maazimio yake.
Wakati Chama cha Mapinduzi (CCM) kikiwa kimeridhia kurudiwa kwa uchaguzi huo, chama kikuu cha upinzani CUF ambacho mgombea wake eif Shariff Hamad anaamini alishinda, kinataka matokeo ya Oktoba 25 yatangazwe.
No comments :
Post a Comment