Maadhimisho hayo hufanyika Januari 27 ya kila mwaka yakishirikisha viongozi wakuu wa chama hicho pamoja na wafuasi wake.
Akizungumza na Nipashe jana, Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho Taifa, Abdul Kambaya, alisema uongozi wa CUF taifa hautafanya maadhimisho hayo kwa kuwa siku hiyo Kamati Ttendaji itakuwa inafanya kikao cha kujadili tarehe ya marudio ya uchaguzi ambayo ilitangazwa hivi karibuni na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec).
Kambaya alisema siku hiyo kamati itakutana kuandaa ajenda kuhusiana na kutangazwa kwa tarehe hiyo ya uchaguzi ambazo zitapelekwa katika Baraza Kuu la chama.“Ni vijana tu ndiyo watafanya maadhimisho hayo kwa upande wa Zanzibar na ndiyo ambao watafanya maandamano ya kukumbuka mauaji hayo.”
Maandamano hayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka kama kumbukumbu ya kuomboleza vifo vya wafuasi wa chama hicho waliouawa Januari 27, mwaka 2001 wakati wa maandamano ya kupinga matokeo ya urais visiwani humo.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment