dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, January 18, 2016

Ushindi wa meya, naibu meya waipa jeuri Ukawa

Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vimeibuka na kusema vilitarajia kushinda katika kinyang’anyiro cha umeya na unaibu meya katika manispaa za Ilala na Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
 
Tambo hizo zimekuja siku moja baada ya kuibuka na ushindi huo ambapo Diwani wa Kata ya Mbezi kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (Chadema), Humphrey Sambo, alisema jana kuwa walitarajia ushindi huo baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana. 
 
Sambo alisema dhamira ya Ukawa ni kuongoza nchi tangu awali, hivyo rasharasha za kuteka majimbo ni miongoni mwa sababu itakayouweka umoja huo madarakani miaka mitano ijayo.
 
“Tunaimani rais wa awamu hii alikuwa Edward Lowassa, lakini nguvu za dola zilichangia kutunyang’anya ushindi huo mikononi. Njama  hizo ndizo zilizokuwa zikitumika kwa viongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao muda mwingi walikuwa wakiutumia kutoa propaganda za uongo kuwahadaa wafuasi wao kujimilikisha  tena viti hivyo.Alisema tangu awali, CCM ilibaini ushindi kwa Ukawa, ila katika harakati za kupiga bao la mkono, walifanikiwa kuwaleta mamluki kupitia chama hicho kutoka Zanzibar na baada ya kubaini, uchaguzi uliahirishwa.
 
Alisema kwa sabubu Ukawa walijiamini hawakuwa na sababu ya kutapatapa kama walivyofanya CCM, na kutumia fursa hiyo kuwashukuru wakurugenzi wa manispaa akiwamo wa Manispaa ya Kinondoni, Kagurumjui Titus, kutumia kanuni na sheria ya uchaguzi katika kutoa haki na kutangaza washindi.
 
Katika kinyang’anyiro hicho, Boniface Jacob wa Chadema, alishinda nafasi ya Meya kwa kupata kura 38, huku nafasi ya naibu Meya ikienda kwa Jumanne Mbunju wa CUF aliyapata pia kura 38. 
 
Kwa upande wa Ilala, nafasi ya Meya ilichukuliwa na Charles Buyeko (Chadema), ambaye alishinda kwa kura 23, wakati Naibu Meya wa manispaa hiyo alichaguliwa Omari Said wa CUF, aliyepata kura 23.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment