'ZEC itimize wajibu wake kwa kufanya majumuisho ya kura na kumtangaza mashindi wa nafasi ya urais wa Zanzibar.'
Msimamo huo ulitolewa jana na Katibu Mtendaji wa JUVICUF Zanzibar, Mahamoud Ali Mahinda, katika taarifa yake ya kuunga mkono msimamo wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, kupinga kurudiwa kwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar.
Alisema uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana ulikuwa huru na wa haki na kuwataka viongozi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) warudi kazini wakamilishe kazi iliyobakia na kumtangaza mshindi wa uchaguzi huo.
“ZEC itimize wajibu wake kwa kufanya majumuisho ya kura na kumtangaza mashindi wa nafasi ya urais wa Zanzibar,” alisema.
Alisema hatua hiyo hitasadia kuepusha Zanzibar kuiingia katika mgogoro wa kisiasa ambao unaweza kusababisha kuchafuka hali ya amani na utulivu.
“Tunakubaliana na uongozi wa CUF hakuna sababu yoyote ya kushiriki katika uchaguzi wa marejeo kwa sababu CUF ilishapewa ridhaa ya kuongoza nchi na wapiga kura halali wa Zanzibar,” alisema.Mahinda aliwataka viongozi wa CCM kuacha kuishinikiza ZEC kuitisha uchaguzi wa marudio badala ya kukamilisha uchaguzi wa Oktoba, mwaka jana.
Alisema kuwa kitendo kilichofanywa na Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha, kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu Zanzibar kimeleta madhara makubwa, ikiwemo kiuchumi na kisiasa, pamoja na kupanda kwa gharama za maisha kwa wananchi.
Aidha, alisema kuwa inasikitisha kuona Zanzibar kumeibuka vitendo vya ubaguzi wa rangi na kufanyika hadharani bila ya wahusika kuchuliwa hatua za kisheria na vyombo vya dola.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment