dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, January 24, 2016

SAIKOLOJIA : Fahamu manufaa ya kuwafanya wengine wajione ni watu muhimu

YOU MUST READ THIS!!! 

By Abeid Sakara, Mwananchi.
Zamani niliwahi kusikia hadithi ya watu wafupi wenye nguvu na waliishi msituni maarufu ‘mbilikimo’. Inasemekana kuwa ukikutana nao njiani anakuuliza, “Umenionea wapi?” Wenye kujua walikuwa wanadanganya kwa kujibu kuwa “Nimekuonea mbali kule” Basi anafurahi na kukupa mkono.
Lakini ukikijibu, “Nimekuonea hapa hapa karibu” anakasirika na kuanza kukupiga mpaka ukimbie.
Unajua kwa nini walikuwa wanakasirika unaposema ulimwona alipofika karibu?
Hii ni kwa sababu walikuwa wanataka waonekane ni watu wakubwa na wa maana.
Binadamu hupenda kuonekana ni mtu mkubwa na wa maana.
Haijalishi kama ni mtu wa mjini au shamba, kama amesoma au hakusoma, mjanja au mjinga muungwana au mtwana, mzee au kijana, kila mmoja hupenda kuonekana mtu wa maana na muhimu.
Hivyo, kila mtu hana budi kutambua kuwa jirani yake, mumewe, mkewe au mtoto wake, bosi wake au mtumishi wake wote wana utashi wa asili wa binadamu wa kuonekana mtu muhimu na wa maana.
Utafiti umethibitisha kuwa haja ya binadamu kuonekana mtu muhimu ni njaa ya kihisia iliyo kubwa kuliko ile ya kibaiolojia ya kutaka kula chakula.
Kuna kisa cha mwindaji wa kijiji fulani aliyerejea nyumbani mbio kuwaarifu wanakijiji kuwa, amemuona mtu aliyevaa parachute akidondoka kutoka angani na kuangukia kwenye kilele cha mlima mrefu msituni.
Watu wote kijijini walishikamana katika juhudi za kumwokoa mtu huyo. Siyo mwindaji wala mtu mwingine yeyote pale kijijini aliyemfahamu mtu huyo au kujua alikotoka.
Hata hivyo, walimshughulikia kwa kuwa yeye kama binadamu ni kiumbe muhimu na wa maana sana.
Pale kijijini hapakuwa mtu yeyote aliyefikiria kwamba kwa kuwa hakukuwa na mtu aliyekuwa akimfahamu kwa hiyo hapakuwa na haja yoyote ya kumshughulikia.
Je, wewe unapotembea barabarani au unapokuwa kwenye daladala, sokoni, madukani au ofisini watu unaokutana nao huwa wanakutazama au kukufikiria namna gani?
Unapowachunguza na kuongea nao huwa unagundua wana mtazamo gani kwako.
Huwa unahisi wanakutazama kama mtu wa maana na muhimu au huwa wanakuona siyo mtu wa maana na wala huna chochote ambacho wanachoweza kunufaika nacho kutoka kwako?
Ingawa kwa kawaida kila binadamu hupenda kuthaminiwa, watu wengi huwatazama watu wengine kwa dharau.
Watu hawa wanafanya kosa kubwa.
Hawana budi kukumbuka kuwa binadamu yeyote, bila kujali hadhi, haiba, elimu au uwezo wake wa kipato ni mtu muhimu kwao.
Kuna manufaa tunapowachukulia wengine kama watu muhimu?
Je, tunapowatazama wengine kama watu muhimu tunapata manufaa yoyote? Jibu la haraka ni kuwa kuna manufaa.
Binadamu huishi katika mfumo wa kijamii. Hivyo, maisha yake hutegemea kushirikiana na watu wengine.
Aidha, ni vyema tuzingatie kuwa, ili wengine watutendee mema na kututhamini, hatuna budi kuwafanya wajione kuwa wao ni watu muhimu.
Kadri tutakavyoongeza hali ya kuwathamini ndivyo kadri wao wanavyoongeza kututhamini na kututendea mema zaidi.
Kuna rafiki yangu na wenzake walikuwa wakipelekwa kazini na kurudishwa nyumbani kwa basi la kazini. Dereva wao alikuwa mtu mzima ambaye hakuwa mcheshi hata kidogo. Alikuwa hana uhusiano na yeyote kati ya abiria wake. Alikuwa akiondoa basi hata kama mtu amebakiza hatua mbili tu kufika kwenye mlango wa basi ati kwa sababu wakati wa kuondoka umefika.
Anasema lakini baada ya muda walistajabu kumwona yule dereva anapatana vizuri na mwenzao mmoja. Hata kama akichelewa kidogo alikuwa tayari kumsibiri hadi afike.
Rafiki yangu na wenzake wakaamua kuchunguza kumetokea nini hadi wapatane hivyo.
Aligundua kuwa yule mwenzao alitumia mbinu ya kumfanya yule dereva ajisikie kuwa yeye ni mtu muhimu.
Kila siku asubuhi alipofika alimsalimu kwa kusema “Habari za asubuhi mzee wangu?” Pia alianza tabia ya kukaa kwenye kiti cha mbele karibu na yule dreva na kumpatia maneno ya kumfurahisha kama vile, “Wewe mzee ni mtu mhimu.
Unatuchukua salama kwenda kazini na kuturudisha nyumbani. Tena wewe ni rubani hodari maana unaliendesha basi hili kubwa kwenye msongamano na foleni na kuhakikisha tunawahi kazini bila kuchelewa.
Alisema kuwa yule mwenzao alikuwa akimwita yule mzee rubani. Kwa sifa hiyo alijiona kama rubani anayeendesha ndege. Jambo hili lilimfurahisha. Matokeo yake akamthamini na kumpenda.
Tunawezaje kuwaonyesha watu kuwa tunawathamini.
Ni muhimu tujiulize tunawezaje kuwafanya watu watuone kuwa tunawathamini.
Moja kati ya mambo haya ni kuwapongeza kuwasifu na kuwashukuru kwa kila wanachotutendea au kutenda kwa ajili ya watu wengine. Tuepuke tabia ya kufikiria kuwa kila tunachotendewa ni haki yetu na tunastahili kufanyiwa.
Pia, kila inapotokea nafasi tuwasifu na kuwapongeza watu kwa mambo kama vile wanavyofanya kazi mawazo yao, tabia zao na mengine mengi.
Jambo jingine ambalo huwafanya watu waone tunawathamini na tunawaona wao ni wa maana ni kuyafahamu majina yao. Watu husema hakuna sauti nzuri anayomfurahia mtu kama jina lake linapotajwa.
Unapoongea na mtu sisitiza mawazo yako huku ukilitaja jina lake.
Kwa kufanya hivyo unamfanya aamini kuwa unamthamini na kumpenda.
Hata hivyo, hakikisha unataja jina ambalo mtu analipenda na epuka kabisa kukosea jina la mtu unapokosea jina la mtu unamfanya aamini moja kwa moja humthamini.

No comments :

Post a Comment