Rais John Magufuli mewaomba mawaziri, manaibu mawaziri, Makatibu wakuu na Manaibu wao wakubali kukatwa Sh. milioni moja kwenye mishahara yao ili zipatikane fedha za ujenzi wa madarasa jijini Dar es Salaam.
Alisema iwapo fedha kutoka kwenye mishahara yao zitakatwa, zitapatikana Sh. milioni 82 na zitabaki Sh. milioni 18 ili zitimie milioni 100 ambazo atazitoa yeye, Makamu wa Rais, Samia Suluhu na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Alisema kuwa anaamini kwasababu yeye ndiye aliyewateua kushika nyadhifa hizo bila kuombwa na mtu yeyote, basi watakubaliana na ombi lake hilo jema ambalo limelenga kuimarisha elimu katika Mkoa wa Dar es Salaam.
“Kwa kuwa niiliwateua mimi mwenyewe na wala sikuombwa na mtu yeyote basi, naamini watakubali kukatwa mishahara ili zipatikane hizo Sh. miloni 82," alisema Rais Magufuli na kwamba "zitakazobaki haiwezi kuwa shida."
Alisema kiasi kilichobaki hakiwezi kuwa tatizo kupatikana "kwasababu mimi nipo, Makamu yupo na Waziri Mkuu yupo, kila mmoja wetu atatafuta Sh. milioni sita ili tutimize milioni 100.”
Mbali na kuchangisha michango hiyo kutoka kwa viongozi hao, Rais Magufuli pia aliahidi kuupatia Mkoa huo Sh. Bilioni 2 kuongeza nguvu ya ujenzi wa madarasa, lakini alionya kuwa watakaojaribu kuzitumia vibaya basi "watakwenda na maji."
“Ntawaongezea Sh. bilioni mbili kwa maana ya milioni elfu mbili, sasa Mkuu wa Mkoa ole wenu atakayejaribu kuzichepusha kwenda kufanya mambo ya ovyo ovyo, nasema kwa dhati kutoka moyoni maana msema kweli mpenzi wa Mungu... mkizichezea mtakiona,” alisema Rauis Magufuli na kusababisha ukumbi kulipuka kwa kicheko.
Aidha, Rais Magufuli alisema Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri ambao kwenye maeneo yao kutakuwa na wanafunzi wanaokaa chini watakuwa wameshindwa kazi na hawatakuwa na uhalali wa kuendelea na nafasi zao.
Alisema haiwezekani kiongozi akakaa kwenye gari zuri, ofisi yenye kiyoyozi na kulala kwenye nyumba nzuri wakati kuna watoto wa watanzania ambao wanakaa chini darasani halafu akaendelea kushika wadhifa wake.
“Hicho kitakuwa kipimo tosha kwamba huna sababu ya kuendelea kuwa Mkuu wa Mkoa, Wilaya ama Mkurugenzi wa Halmashauri," alisema.
"Mkiona wanafunzi wanakaa chini mtakuwa mmeshindwa kazi na ni heri mkapisha ili watakaoweza kukabiliana na changamoto hizo wakalie hizo ofisi.
“Tanzania hii inautajiri wa kila aina, hakuna sababu kwa wanafunzi kukaa chini wala wagonjwa kulala wawili wawili kitandani, haiingii akilini kila ukipita sehemu ni shida tu wakati tuna rasilimali za kila aina, lazima viongozi tuwajibike kuondoa chanagamoto hizi kwasababu uwezo tunao na atakayeona hawezi apishwe wengine wanaoweza.”
Kufuatia kuanza kutimizwa kwa ahadi ya Rais Magufuli ya Elimu Bure kuanzia daraa la awali mpaka kidato cha nne mwaka huu, shule nyingi, hasa za mkoa wa Dar es Salaam zimekumbwa na ongezeko kubwa la wanafunzi.
Katika baadhi ya shule, idadi ya wanafunzi walioandikishwa kwa mara ya kwanza imezidi maradufu wanafunzi wote waliokupo wa darasa la kwanza mpaka la saba.
Shule ya Msingi Majimatitu ya Temeke jijini Dar es Salaam, kwa mfano, imeingia kwenye rekodi ya aina yake hapa nchini na pengine Afrika kutokana na kusajili wanafunzi 1,022 wa darasa la kwanza. Idadi ambayo inatosha kuanzisha shule nyingine.
Idadi hiyo imeifanya Majimatitu kuwa na jumla ya wanafunzi 6,000.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa shule hiyo ndiyo inayoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaosomea chini ya miti.
Shule hiyo ina madarasa 22 na ili iweze kumudu idadi hiyo ya wanafunzi wa darasa la kwanza mpaka la saba inahitaji nyongeza ya madarasa 109. Aidha inatakiwa kuwa na matundu 239 ya choo lakini kwa sasa yako matundu 36 tu.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments :
Post a Comment