Msemo wa waswahili kwamba ng’ombe wa maskini hazai unaonekana kuwa kweli kwa Shirika la Ndege Nchini (ATCL), ambalo ndege yake pekee imenusurika kuwaka moto katika uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam juzi.
Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa wakisafiri kwenda mataifa mbalimbali ambao walizungumza na Nipashe juzi jioni, ndege hiyo ilionekana ikitoa moshi mwingi hali iliyosababisha magari ya zimamoto kufika eno hilo ili kuzima moto.
Msafiri mmoja ambaye alikuwa akipanda ndege kuelekea Nairobi, Kenya aliliambia gazeti hili kuwa waliona ndege hiyo ya ATCL ikitoa moshi mwingi hali iliyoashiria kuwa kulikuwa na hitilafu kwenye injini yake.
“Tuko hapa na tunaiona ndege inatoa moshi kweli kweli, watafuteni wahusika wawaambie tatizo nini,” alisema abiria huyo ambaye baadaye alituma picha mbalimbali za mnato na video kwa njia ya simu zikionyesha ndege hiyo ikitoa moshi mwingi.
Gazeti hili liliwasiliana na Katibu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini, Ramadhani Maleta, ambaye alisema hawezi kulizungumzia suala hilo na alielekeza watafutwe wahusika wakuu ambao ni ATCL.
“Mimi siyajui hayo na wala siwezi kuwasemea wakati wenyewe wapo, watafuteni ATCL wao ndiyo wanauwezo wa kulizungumzia kwa kina suala hili, mimi kwanza siko kazini muda mrefu,” alisema Maleta.
Alipoulizwa kuhusu hitilafu ya ndege hiyo, Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga, TCAA, Bestina Magutu, aliliambia gazeti hili kuwa ni vyema suala hilo wakaulizwa wahusika ambao ni ATCL kwa kuwa yeye si msamaji wa shirika hilo.
Jitihada za kumpata msemaji wa ATCL hazikuzaa matunda jana.
Akizungumza wakati wa siku ya sheria nchini, Rais John Magufuli alielezea kushangazwa kwake na kudumaa kwa ATCL hata kushindwa kumudu kuwa na ndege zake kama yalivyo mashirika mengine ya ndege Afrika na duniani.
Rais Magufuli alisema ana uwezo wa kununua hadi ndege sita mpya za kuliendesha shirika hilo lakini lazima wapatikane watumishi ambao watakuwa na uwezo wa kuliendesha na ikiwezekana "kuwafuta wafanyakazi wote walioko sasa."
Moja ya ndege za shirika hilo yenye namba FT 119 iliwahi kushindwa kupaa katika uwanja wa ndege wa Kigoma, Aprili mwaka 2012 na kuserereka hadi mwisho wa uwanja huo kisha kunasa kwenye tope, na bawa lake la kulia kukatika.
Ingawa hakuna watu waliofariki kwenye ajali hiyo, lakini abiria kadhaa walijeruhiwa na wengine walipata mshtuko wa hapa na pale kutokana na mkasa huo.
Ndege hiyo iliyokuwa na abiria 35 na wafanyakazi wanne ilikuwa ikiruka kuelekea jijini Dar es Salam kupitia Tabora lakini katika harakati za kuruka ilishindwa na kuserereka hadi nje ya uwanja sehemu iliyokuwa na matope na kunasa.
Shirika hilo lilisema kuwa, ndege hiyo haifai tena kwa ajili ya kubeba abiria.
Miaka ya nyuma shirika hilo lilikuwa likitoa huduma bora za usafiri wa ndege katika maeneo yote nchini na kimataifa likiwa na safari za barani Afrika na Ulaya.
Mwaka 2010 ATCL ilipata janga lingine baada ya ndege ya kukodi ya shirika hilo aina ya Boeing 737 iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kupata ajali ndogo wakati ikitua katika Uwanja wa Mwanza, ikiwa na abiria wanaokadiriwa kuwa 46.
Ndege hiyo ilipata ajali hiyo wakati ilipotua kwenye uwanja uliojaa maji kutokana na mvua kubwa iliyokuwa imenyesha hivyo kuserereka hadi nje kabisa ya njia ya kutua na kurukia ndege.
Tangu mwaka 2010 ndege hiyo haijaondolewa eneo hilo na serikali haijasema inatarajia kuifanyia nini ndege hiyo.
ATC kabla ya kuitwa ATCL lilianza na ndege 11 ilizopata baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya kwanza ya Afrika Mashariki (EAC) mwaka 1977.
Rwanda mwanachama mpya katika EAC na nchi ambayo haina rasilimali nyingi kama Tanzania, kwa sasa ina ndege kubwa nane zinazotoa usafiri wa uhakika katika nchi mbalimbali za Afrika na nje ya bara.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments :
Post a Comment