Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, February 12, 2016

Wasomi, wanasiasa wamchambua Magufuli!

Rais Dk. John Magufuli
Wakati Rais Dk. John Magufuli akitimiza siku 100 leo, wasomi na wanasiasa wamemwelezea walivyomwona katika kipindi hicho.
Nipashe ilizungumza na baadhi ya wasomi hao ambao walimwelezea kuwa ni Rais aliyedhamiria kuibadilisha Tanzania, kupambana na rushwa na kuziba mianya ya ukwepaji kodi.
Mhadhiri Chuo cha Diplomasia, Israel Sosthenes, alisema kwa sasa ni mapema kumwelezea Rais Magufuli kwa siku 100 alizofikisha akiwa madarakani.
 
Alisema uhusiano wa kidiplomasia unajengwa kwa muda mrefu na si katika kipindi cha siku 100.
 
“Kwa mujibu wa mkataba wa Vienna wa uhusiano katika masuala ya kidiplomasia wa mwaka 1961, Rais ndiye mwakilishi wa nchi na ndiye mwanadiplomasia namba moja katika nchi,” alisema Sosthenes.
 
Alisema Rais ndiye anayepaswa kuiwakilisha nchi katika mikutano ya kikazi na kirafiki kwa nchi zilizoingia ubia au uhusiano wa kimataifa.
 
Hata hivyo, alisema Rais anaweza kuwakilishwa na  Waziri Mkuu, Mkamu wa Rais, Waziri wa Mambo ya Nje au balozi wa nchi husika anayotakiwa kwenda.Alisema kwa siku 100 Rais ameweza kufungua ubalozi nchini Kuwait, amepokea hati ya utambulisho kwa mabalozi wa Umoja wa Ulaya, Oman, Qatar pamoja na kufungua ubalozi nchini Brazil, hivyo ni uhusiano wa kidiplomasia tosha aliyoyafanya.
 
Alisema serikali ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere ilijenga uhusiano mazuri na nchi za nje, hata serikali ya awamu ya nne ya Jakaya Kikwete nayo ilijenga uhusiano mkubwa kwa kusafiri sana, hivyo Rais Magufuli hana haja ya kusafiri kwa uharaka kwa sasa.
 
Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Namibia, Idara ya Uandishi wa Habari, Julius Mtemahanji, alisema  siku 100 za Rais Magufuli zimedhihirisha utofauti wa uongozi baina yake na watangulizi waliotangulia.
 
Alisema kutosafiri nje ya nchi ni jambo la busara kwa sababu ameonesha kuwajali wananchi wake ambao wamekuwa wakitaabika kwa miaka mingi kwa kutokuwa na huduma za kijamii, huku marais watangulizi wakitumia mabilioni kwenda nje ya nchi.
 
Naye mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Dk.Kaiza Bubelwa alisema katika siku 100 Rais Magufuli ameonyesha matumaini makubwa kwa watanzania.
 
Alisema hadi sasa ameshawaajibisha watendaji waliotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi serikalini na mashirika ya umma. Rais Magufuli ameonyesha wananchi na wasaidizi wake msimamo wake juu ya rushwa, uzembe na ifisadi.
 
Alisema Rais Magufuli  atakuwa Rais asiye na suluhu kwa uzembe, rushwa, ufisadi na matumizi masiyofaa ya pesa za umma. Alisema amekwishabainisha  kuwa sifa ya kiongozi kuendelea kuhudumu serikalini sharti awe mwadilifu na mkweli. 
 
Aliyekuwa mgombea Urais kupitia Chama Cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira, alisema Rais Magufuli ameweza kusaidia ongezeko la makusanyo ya kodi kutoka Sh. bilioni 800 hadi Sh. Trilioni 1.4 kwa mwezi.
 
Alisema Rais Magufuli ni kiongozi aliyeonyesha utofauti mkubwa kati yake na viongozi waliopita kwa kuweza kuwaadabisha viongozi wazembe.
 
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Nicholaus Mgaya, alisema kwa simu 100 wanaridhishwa na utendaji kazi wa Rais Dk. Magufuli kwa kuwa kilio cha wafanyakazi kwa muda mrefu ilikuwa kukusanya kodi kwa wafanyabiashara na kubana matumizi.
 
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Onesmo Olengurumwa, alisema Dk. Magufuli amefanikiwa kupambana na rushwa ndani ya siku 100 ameonyesha mwanga.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment