Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga wakisali katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita. Rais Dkt. Magufuli amesali ibada ya jumapili ya pili ya Pasaka tangu kuchaguliwa kuwa Rais.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Mke wa Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya, Bi. Ida Odinga, Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Raila Odinga pamoja na Rais Dkt. John Magufuli wakifatilia kwa makini mahubiri yaliyokuwa yakitolewa katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.
Kikundi cha Kwaya ya vijana wakiimba katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono kutakiana amani ya bwana na masista wa kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Raila Odinga pamoja na Mke wa Raila Bi. Ida Odinga wakifatilia kwa makini mahubiri ya Paroko Padre Henry Mulinganisa katika ibada ya pili ya pasaka Chato Mkoani Geita.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Sakramenti takatifu kutoka kwa Paroko wa Parokia ya Bikira Maria Chato Padre Henry Mulinganisa .
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisali katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisali katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia waumini wa kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita. Rais Dkt. Magufuli amechangia kiasi cha Shilingi milioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa jipya la la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.
Mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga akiwasalimia waumini wa kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Mke wa Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya, Bi. Ida Odinga pamoja na Rais Dkt. John Pombe Magufuli wakifurahia salamu zilizokuwa zikitolewa na Raila Odinga katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Raila Odinga, Mke wa Raila Bi. Ida Odinga pamoja na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wakishukuru mara baada ya ibada.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Raila Odinga wakiagana na waumini wa kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Sista Maria Theleza Ntihabose wa kanisa la la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita. Picha na Ikulu.
No comments :
Post a Comment