Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi (wa tatu kushoto) akiongoza matembezi ya hisani Sept 17, 2016 kuchangia wahanga wa tetemeko lililotokea Septemba 10 2016.
Photo Credits: Mohammed Mambo / Daily News
Akiwa na miaka 91 sasa, Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi bado anaonekana mwenye nguvu na afya njema, na amekuwa akishiriki maandamano (pengine) kuliko kiongozi yeyote mkubwa wa kiTaifa nchini Tanzania.
Lakini hili si suala ambalo linakuja kirahisi. Mzee Mwinyi amekuwa makini katika chakula na pia amekuwa akifanya mazoezi sana.
Mei 8 2015 tulipata kuchapisha mahojiano kati yetu naye alipokuwa akiadhimisha miaka 90. Na mbali na mengi aliyozungumzia katika kuakisi miongo 9 ya uhai wake, pia alizungumzia kuhusu SIRI ya afya bora aliyonayo.
Alisema kwamba hahudhiki kirahisi. Pia amesema kwamba a"nafanya mazoezi sana. Kila siku. Mpaka leo, sina siku hata moja, labda nije huku Marekani. Lakini sina siku hata moja nisiyokwenda mwendo wa kati ya kilometa tano hadi saba kila asubuhi. Na inanichukua saa moja. Halafu, nina baiskeli, ninaendesha kwa muda wa nusu saa kila siku"
Pia alitoa ushauri kwa vijana akisema "wachague vyakula. Wasile vyakula vyovyote tu vile. Na exercises wafanye sana......na hivi vinywaji navyo vinavyofurahisha, vinavuruga afya ya mtu"
No comments :
Post a Comment