Kikundi cha Mungu Hamuachi Mja Wake kilichopo kangani shehia ya kukuu wilaya ya mkoani, mkoa wa kusini Pemba wameiomba serikali iwasaidie kiasi cha shilingi milioni 20 ili kukidhi mahitaji yao.
Hayo yameelezwa na mshika fedha wa kikundi hicho ndugu Kazija Sudi Juma wakati akizungumza na mwandishi mwandishi wa haabri hizi juu ya faida na changamoto zipatikanazo katika vikundi mbalimbali vya ushirika.
Kazija amesema,harakati katika kikundi chao zinakwenda lakini ni katika mwendo wa kinyunga ambapo amesema serikali,taasisi za kiraia na mashirika mbalimbali kujitokeza kwa lengo la kuwapa msaada kwakua wanahisi hali inazodo kudorora na wameshawahi kutafuta misaada bila ya mafanikio.
Msaidizi mwenyekiti wa kikundi hicho ndugu Zuwena Abdalla amesema kuwa katika kikundi chao kuna matatizo ya vifaa kama vile keni ya kumwagilia maji pamoja na pembejeo tofauti ambazo ni muhimu katika kuendeshea kazi zao.
Msaidizi mwenyekiti wa kikundi hicho ndugu Zuwena Abdalla amesema kuwa katika kikundi chao kuna matatizo ya vifaa kama vile keni ya kumwagilia maji pamoja na pembejeo tofauti ambazo ni muhimu katika kuendeshea kazi zao.
Amesema kuwa serikali iwaangalie kwa jicho la huruma sambamba na kujikwamua kimaisha ili kuepukana na umaskini.
Wanakikundi hicho kwa pamoja wamewashauri vijana nchi kutokaa mitaani ovyo wakasingizia kutoka na ajira na badala yake wajikurupushe na ikiwezekana waunde kikundi cha ushirika katika kazi watakayoiona wao inafaa ikiwa ni kilimo, ufugaji au ujasiriamali mwengine kwa lengo la kufanya kazi kwa pamoja na hatiame kujikwamuga na hali ngumu ya kimaisha.
Wamesema kufanya hivyo kutawasaidia kutojiingiza katika janga baya la wizi,utapeli na utumiaji wa madawa ya kulevya.
/Salmin J Salmin
No comments :
Post a Comment