Dar es Salaam. Jukwaa la Katiba Tanzania limemtaka Rais John Magufuli kuendelea mchakato wa Katiba Mpya kama CCM ilivyoahidi kwenye ilani ya uchaguzi.
Akizungumza leo mratibu wa jukwaa hilo, Hebron Mwakagenda amesema kauli ya Rais kwamba hakuwaahidi wananchi kwenye kampeni kuwa ataendeleza Katiba ni sawa na kukikana chama chake.
Amesema mchakato wa Katiba umetumia Sh 100 bilioni za walipakodi na kwamba usipoendelezwa ni sawa na dhuluma kwa wananchi.
No comments :
Post a Comment