dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 18, 2016

Barua ya Mohammad Ali kwa Mandela Yauzwa Milioni 19.58!

 

Barua iliyowekwa sahihi na mwanamasumbwi Mohammad Ali na kuandikiwa rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, akitoa rambi rambi zake kufuatia kuawa kwa mtu aliyekuwa akipinga ubaguizi wa rangi imeuzwa kwa pauni 7,200 sawa na Tsh. 19,577,911.

Muuzaji wa barua hiyo Andrew Aldridge alisema, “ni vyema kuwa Mohammad Ali alikuwa mwanamichezo bora zaidi hukui naye Nelson Mandela akiwa mtu mashuhuri zaidi katika karne iliyopita.”


 
Barua hiyo ilipewa Chapa cha Msaidizi wa Meneja wa Hoteli ya Elangeni iliyo mjini Durban ambapo Ali alikuwa akiishi wakati huo.

Barua hiyo iliyouzwa kwa mnunuzi kutoka nchini Marekania ilitarajiwa kuuzwa kwa kati ya dola 6,000 na 8,000.

Chris Hani(KUSHOTO) akiwa na Nelson Mandela.

Muhammad Ali alikuwa nchini Afrika Kisini kwa kipindi kifupi mwezi Aprili mwaka 1993 baada ya kuwasili muda mfupi baada ya kuuliwa kwa Chris Hani tarehe 10 mwezi Aprili.

Hani alikuwa kamanda wa kundi la Umkhonto We Sizwe, kundi lililojihami la ANC.

Alikuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya ubaguzi wa rangi na aliuaw mkereketwa mmoja nje ya nyumba yake eneo la Boksburg.

No comments :

Post a Comment